Babu Seya kulia na Mwanae Papii Kocha |
Studio kubwa ya Mziki hapa
Tanzania na Afrika Mshariki, Wanene Studios imeamua kubeba jukumu la
kuwarudisha kwenye anga za maziki wa Dansi waimbaji maarufu Nguza Viking “ Babu
Seya” pamoja na mwanae Johnson Nguza “Papii
Kocha”
Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na
Michezo, Bi. Juliana Shonza aliwakutanisha na uongozi wa Studio hiyo.
Itakuwa ni mara ya kwanza , wameanza
maandalizi ya ujio wao mpya, ikiwa ni takribani miaka 14 tangu waachie kibao
kipya.
Wawili hao walipewa msamaha na Rais Dkt John Magufuli kwenye
maadhimisho ya miaka 56 ya Uhuru. Serikali imeonesha nia ya kuwasaidia waimbaji
hao wanaopendwa sana kurejea tena kwenye muziki kwa kishindo.
Tayari wameanza kuingia studio kuandaa kazi mpya katika studio
hizo kubwa na bora zaidi katika ukanda wa Afrika Mashariki na kati. Wameanza
kwa kufanya photoshoot, kitu ambacho wamekiri kuwa ni kigeni mno kwao kutokana
na kuwa gerezani kwa miaka 14 na wametoka katika nyakati ambazo muziki wa
Tanzania umepiga hatua kubwa ukilinganisha na zamani.
“Miaka 14 si mchezo, mambo kama haya si unayaona mwenyewe,
niliyamiss, nimemiss vitu vingi, picha za ukweli, mambo haya kule tulipotoka
hamna. Lazima uelewe hii ni dunia nyingine,” alisema Papii Kocha wakati wa
photoshoot.
Kwa kujiamini, Papii amesema kuwa kazi zao mpya zitakuwa kali
zaidi ya zile za zamani. “Kwasababu tumejipanga vizuri na kazi zinazokuja
zitakuwa nzuri zaidi ya zile tulizofanya mwanzo,” amesisitiza Papii. Kwenye
photoshoot hiyo iliyofanywa na mpiga picha mahiri Eric Luga, Babu Seya na Papii
Kocha walivalishwa na mbunifu wa mavazi, Mtani Nyamakababi.
No comments:
Post a Comment