Emmanuel Kibiki Mwandishi wa Raia Mwema- Njombe (Picha ya Mtandao) |
Kukiwa bado Watanzania tuna kumbukumbu ya mwandishi wa Habari Azori Gwanda hajapatikana, Kundi kubwa la Askari
Polisi Wamevamia na kupekua nyumbani kwa Mwandishi wa habari wa Raia Mwema
Emmanuel Kibiki, kuanzia saa 6 usiku hadi 9 alfajiri na baadaye kuondoka naye.
Mwandishi huyo amekuwa akifanya kazi zake mjini Makambako
Njombe, alivamiwa na askari hao ambao idadi yao haikajulikana na kulazimisha
kuingia ndani kufanya upekuzi.
Habari zilizothibitishwa na Mhariri wa gazeti la Raia Mwema,
Ezekiel Kamwaga zinaeleza, mwandishi huyo alizuia askari hao kuingia na kufanya
upekuzi bila kufuata taratibu.
Anaeleza: Nimepigiwa simu na mkewe, Tobina, akilia machozi kuwa
mumewe alifuatwa na askari hao majira ya saa sita usiku wa kuamkia leo.
"Tulikuwa tumelala mara tukasikia mlango unagongwa.
Kufungua tukaona ni askari polisi waliokuja na magari mawili. walikuwa ni
askari wengi mpaka ilitisha. Sikuwahesabu lakini walikuwa wengi.
"Wakasema wanataka kupekua ndani. Mume wangu akawagomea.
Akawauliza kama wana kibali cha kumpekua. Hawakuwa nacho. Kibiki anasoma masomo
ya sheria kwa sasa na alishindana nao kwa hoja na Ikawa rabsha mpaka akaja
mjumbe wa serikali ya mtaa. Polisi wakaruhusiwa kumpekua kuanzia saa sita mpaka
saa tisa.
"Walisema wamepata maelekezo kutoka juu na kosa lake ni
kwamba anaandika sana mambo ya siasa na waliowatuma hawapendi. Wamemchukua
tangu saa tisa usiku na hajarejea mpaka muda huu," Tobina amenieleza kwa
kilio cha kwikwi muda mchache uliopita.
Tobina na mumewe wanaishi Makambako Mjini katika eneo la
Mwembetogwa. Kibiki ni mwandishi wa habari wa muda mrefu na hujulikana pia kwa
lakabu (jina la utani) ya Yo Man. .
Amekuwa akiandika mawazo yake katika mitandao ya kijamii na
magazeti mbalimbali likiwamo Raia Mwema.
No comments:
Post a Comment