Weah ameapishwa
kuchukua nafasi rais wa kwanza mwanamke barani
Afrika ,Bi.Ellen Johnson Sirleaf, ambaye amestaafu.
Kuingia kwa Weah
madarakani kunakamilisha shughuli ya kwanza ya amani ya mpito nchini humo tangu
mwaka 1944.
Sherehe hiyo imehudhuriwa
na viongozi wa mataifa kadha pamoja na nyota wa kandanda duniani.
Akihutubia
baada ya kula kiapo, Bw Weah amesema:
"Nimekuwa katika viwanja vingi maishani, lakini sijawahi kuhisi
hivi."
Ameahidi
kujitolea kuwatumikia raia wa nchi hiyo.
"Nitafanya
zaidi ya mchango ninaotarajiwa kutoa ili kutimiza matarajio yenu - lakini
naomba nanyi mtimize matarajio yangu, siwezi kutimiza haya peke yangu."
Kiongozi
huyo ametumia hotuba yake kusifu uhusiano wa karibu kati ya taifa hilo na
Marekani na China.
Kadhalika,
amezungumza kuhusu Umoja wa Ulaya.
Amesema:
„Bila bara la Ulaya, Weah hangekuwa
amesimama hapa leo."
Weah alicheza mpira wa miguu katika klabu kadha za Ufaransa na
Uingereza miaka ya 1980 na 1990 na akaibuka Mwafrika wa kwanza kushinda tuzo ya
Fifa ya Mchezaji bora wa mwaka duniani na tuzo ya Ballon d'Or.
Didier Drogba kutoka Ivory Coast ni miongoni mwa wachezaji
mashuhuri ambao wamehudhuria sherehe hiyo katika uwanja wa Samuel Doe viungani
mwa mji wa Monrovia.
Weah aliingia katika siasa baada ya kustaafu soka mwaka 2002 na
akawa miongoni mwa maseneta katika bunge la Liberia.
Aligombea urais mwaka 2005, na alimshinda Bi Johnson Sirleaf
wakati wa duru ya kwanza katika uchaguzi huo lakini akashindwa katika duru ya
pili ambapo kambi yake ilisusia kushiriki katika duru ya pili.
No comments:
Post a Comment