Imeelewa kuwa kuna magogo hayo 938 yamekuwa bandarini hapo kwa miaka 10 na mengine kwenye makontena 55 yapo hapo kwa miaka miwili hayana mwenyewe mpaka sasa.
Hayo yamesema na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt Hamisi Kigwangalla amesema magogo 938 yaliyopo katika Bandari ya Dar es Salaam yatauzwa wakati wowote baada ya wamiliki wake kutojitokeza.
Mwezi
uliopita, Kigwangalla alifanya ziara ya kushitukiza bandarini hapo baada ya
kupata taarifa kuwa kuna shehena hiyo ya magogo ambayo umiliki wake ulikuwa na
utata.
.
Kutokana na
utata huo, Kigwangalla alitoa siku 30 kwa wamiliki wa makontena 55 kujitokeza
wakiwa na nyaraka zote ili kuthibitisha kama kweli yalivunwa Zambia kama
ilivyodaiwa.
Alisema
kushindwa kujitokeza na kuthibitisha hilo ndani ya muda waliopewa, magogo yote
yangetaifishwa na kuwa mali ya serikali. Alipoulizwa kuhusu hatma ya magogo
hayo baada ya siku 30 alizotoa kwisha, Waziri Kigwangalla alisema kuwa hakuna
mtu yeyote aliyejitokeza kuthibitisha umiliki wake.
“Kulikuwa na
vikao mbalimbali ndani ya serikali kujadili suala hilo, na tumekubaliana
kuyauza baada ya wahusika kutojitokeza kuthibitisha umiliki wake,” alieleza
Waziri. Alisema jukumu la kuyauza magogo hayo wamepewa Mamlaka ya Mapato nchini
(TRA) wanaoruhusiwa kisheria kufanya kazi hiyo.
TRA
watashirikiana na Wakala wa Huduma za Misitu nchini (TFS). Alisema siku rasmi
ya kuuzwa kwa magogo hayo itajulikana hapo baadaye baada ya taratibu zake
kukamilika. Mtendaji Mkuu wa TFS, Profesa Dos Santos Silayo alisema magogo ambayo
yako kwenye mpango wa kuuzwa ni 938.
Yaliyomo
kwenye makontena 55 hayatauzwa kwa sasa kwa kuwa kuna kesi ya msingi na
uchunguzi unaendelea. Prof Silayo alisema thamani halisi ya magogo 938
haijulikani, kwa kuwa wamiliki wake ambao wana nyaraka za mzigo huo
hawakujitokeza.
Alisema
kutokana na hali hiyo, thamani ya magogo hayo itajulikana baada ya tangazo la
kuuzwa kutoka. Alisema tangazo litakapotoka watapata fursa (TFS) ya kupima gogo
moja moja ili kujua ukubwa wake, aina ya mti na ndipo thamani ya magogo yote
itakapojulikana.
Awali, Waziri
alisema taarifa za kiintelejensia alizopata, zinadai magogo hayo mara nyingi
huvunwa Rukwa na kisha kupitishiwa nchini Zambia halafu huingizwa tena hapa
nchini. Alisema watu hao wakiwa Zambia husema magogo hayo wameyavuna Tanzania
na wakiwa Tanzania husema wameyavuna nchini Zambia.
Kutokana na
sintofahamu hiyo, aliagiza wamiliki wajitokeze na nyaraka zinazoonesha kweli
magogo hayo yalivunwa nchini Zambia na uhalali wa umiliki wao, lakini
hawakutokea. Kuhusu matumizi ya magogo hayo, Waziri alisema hutumika
kutengeneza vitu mbalimbali kama vile samani, dawa pamoja na marashi
No comments:
Post a Comment