Mahakama ya Ilala
jijini Dar es salaam leo Jumatatu Januari 22,2018 imemhukumu Mwalimu wa Sanaa
ya kujihami, 'Martial arts' Salum Njwete maarufu kama Scorpion, kutumikia
kifungo cha miaka saba jela na faini ya Sh milioni 30.
Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Ilala,
Flora Haule baada ya Scorpion (35) kupatikana na hatia katika kesi ya kujeruhi
ikiwemo kumtoboa macho kinyozi, Said Mrisho.
Hata
hivyo mahakama hiyo ilimuachia huru kwa kosa la unyang'anyi wa kutumia
silaha.
Oktoba
31,2017, Mahakama hiyo ilisema Salum Njwete ana kesi ya kujibu ambayo ni
unyanganyi wa kutumia silaha na kujeruhi.
Scorpion
alidaiwa kutenda kosa alilohukumiwa nalo Septemba 6,2016 katika eneo la
Buguruni Jijini Dar es Salaam.
Upande
wa mashitaka katika kesi hiyo ulikuwa na mashahidi 10 huku Mshitakiwa aliyekuwa
akitetewa na Wakili Juma Nassoro alikuwa na mashahidi wawili.
No comments:
Post a Comment