Wabunge
sasa wemeoneshwa kukerwa na Mkataba wa Mradi wa Mlimani City na wameiomba
Serikali kuuvunja kwani haukinufaishi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM)
badala yake unamnufaisha mwekezaji Kampuni ya Mlimani Holding Limited (MHL).
Wakichangia
Taarifa ya Shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) ya
Mwaka 2017 bungeni jana, walisema mkataba huo hauna maslahi kwa ‘UDSM’ hivyo,
ni heri uvunjwe.
Mbunge wa Iramba Mashariki, Allan Kiula (CCM) alisema, UDSM
hainufaiki na Mkataba huo, kutokana na mwekezaji huyo kuwekeza fedha kidogo
kiasi cha Dola za Marekani 75 sawa na Sh 150,000, lakini pia kukimbilia Kituo
cha Uwekezaji Tanzania (TIC) ili kupata msamaha wa mwekezaji.
“Mwekezaji
amekuwa hayaendelezi maeneo ambayo yangekinufaisha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,
badala yake amekuwa akiendeleza maeneo anayonufaika nayo yeye,” alisema Kiula.
Alisema, kitu cha ajabu wabia wa mradi huo, wamekuwa wakigawana salio, kitendo
kinachoonesha wanapata faida, lakini faida hiyo haiendi UDSM.
Alisema katika
kipindi cha miaka 13 tangu mkataba uingiwe, mradi wa ujenzi wa hoteli ya nyota
tatu yenye vyumba 100 bado haujaanza kinyume na makubaliano, hivyo kuongeza
gharama za kumalizika mradi.
Mbunge wa
Viti Maalumu, Munde Tambwe (CCM), alisema serikali inatakiwa kufuta Mkataba huo
japo ni wa miaka 85, kwani ni mbovu unaomnufaisha mwekezaji pekee. Mbunge wa
Viti Maalumu, Catherine Ruge (Chadema), alisema mkataba huo una maajabu saba na
moja ya majabu hayo ni kwamba, mmiliki wake hajawahi kufika nchini na hivyo
anatuma watu kuangalia maendeleo ya mradi huo.
Akiwasilisha
taarifa ya Kamati hiyo, Mwenyekiti wa Kamati, Naghenjwa Kaboyoka aliishauri
serikali kumwomba Mkaguzi na Mdhibiti wa Fedha za Serikali (CAG) kufanya
ukaguzi wa kiuchunguzi katika mchakato mzima wa mkataba huo.
Koboyoka alisema,
kutokana na makubaliano ya ujenzi wa Mradi wa Mlimaji City ulioanza Oktoba 1,
2004, ukitakiwa kukamilika Septemba 01, 2006, kwa makubaliano ya mkodishaji
(UDSM) na mkodishwaji (kampuni ya Mlimani Holding Limited) mradi huu bado
haujakamilika hadi sasa.
Uchambuzi wa
Kamati kupitia taarifa ya CAG pamoja na mahojiano na uongozi wa UDSM, umebaini
dosari kubwa katika usimamizi na uendeshaji wa mradi huo, hali unaiyofanya
serikali iendelee kupata hasara.
“Upungufu
uliopo katika mkataba huo, unainyima Serikali mapato stahiki hivyo kuwa na eneo
mojawapo lenye matumizi mabaya ya fedha za umma,” alisema
. Kuhusu Mradi wa
Dege, Kigamboni, Kamati imebaini kwamba mradi wa ujenzi wa Dege Eco Village
unaotekelezwa na Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) umekwama kukamilika kwa
wakati, hivyo Bunge linaishauri serikali ikamilishe haraka mradi huo ili kuokoa
fedha za umma zinazowekezwa katika mradi huo.
Kuhusu
ununuzi wa magari yenye thamani ya Dola za Marakeni 29,606,100 uliofanywa na
Jeshi la Polisi bila kuwepo wa mkataba, taarifa ya CAG imebaini dosari kubwa
katika mchakato wa ununuzi wa magari 777 uliofanywa na jeshi hilo ikiwa ni
pamoja na manunuzi kufanyika bila uwepo wa mkataba.
No comments:
Post a Comment