Daktari akimfanya vipimo kwa mgonjwa w Saratani Wanasayansi wamepiga hatua kubwa katika matibabu ya binadamu kwa kupata kipimo cha damu kinachogundua aina tofauti za Saratani |
Timu ya
Watafiti kutoka Chuo Kikuu cha Johns Hopkins wamefanyia utafiti njia ambazo
zinaweza kugundua aina nane zinazosababisha ugonjwa huo.
Watafiti
hao kutoka Uingereza wanasema mtu anapaswa kufanyiwa uchunguzi kwa mwaka, ili
kuweza kugundua ugonjwa wa Saratani mapema na kuweza kuokoa maisha yake. Huku
wakisifia matokeo ya utafiti wao.
Uvimbe
hutokea na kuonesha dalili kwamba ni ugonjwa wa Saratani hutoa viashiria vidogo
vya vinasaba -DNA- zilizobadilika pamoja na protein kwenye mfumo wa damu.
Watafiti hao kutoka Uingereza wanasema mtu anapaswa kufayiwa
uchunguzi kwa mwaka, ili kuweza kugundua ugonjwa wa Saratani mapema na kuweza
kuokoa maisha yake. Huku wakisifia matokeo ya utafiti wao.
Kwa
ujumla vipimi vya utafiti huo hupata asilimia 70 ya Saratani.
Akizungumzia
suala hilo Dokta Cristian Tomasetti
kutoka Chuo Kikuu cha Johns Hopkins amesema hatu ya kutambua ugonjwa wa
Saratani mapema ni muhimu na matokeo ni ya kusisimua.
Saratani
inapogundulika mapema inakuwa na nafasi kubwa ya kuweza kuitibu.
Wataalamu
wanasema pia kwa baadhi ya wagonjwa matibabu yanaweza kuwa mabaya zaidi kuliko
kuishi na saratani yenyewe ambayo haiatarishi haraka maisha.
No comments:
Post a Comment