Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis leo anahitimisha ziara yake nchini Chile kwa kufanya ibada ya wazi kwenye ufukwe kabla ya kuelekea Peru, nchi ya mwisho kwenye ziara yake hiyo katika bara la Amerika ya Kusini.
Mahubiri ya Papa kwa maelfu ya waumini wanaotarajiwa kwenye ufukwe wa Lobitos karibu na mji wa kaskazini wa Iquique yatalenga zaidi masuala ya wahamiaji. Ukiwa kilometa 1,800 Kaskazini mwa mji mkuu - Santiago, mji wa Iquique umekuwa njia muhimu ya wahamiaji haramu kutoka mataifa maskini yanayoizunguka Chile, na kusaidia kuendesha uchumi.
Kufuatia ibada ya leo kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki mwenye miaka 81 atakutana na waathirika wa ukatili wa dikteta Augusto Pinochet kati ya mwaka 1973-1990 kabla ya kuelekea katika mji mkuu wa Peru, Lima leo jioni.
Maandamano ya kupinga unyanyasaji wa kingono wa kanisa na mashambulizi dhidi ya makanisa yalitawala ufunguzi wa ziara yake.
No comments:
Post a Comment