Wakazi cha kijiji cha Kirichu kaunti ya Nyeri nchini Kenya walishangazwa na wezi waliojaribu kufukua mwili kwa nia ya kuiba jeneza la thamani ya Kshs 80,000 (Takribani Tsh16,000,0000)
Mwanamke aliyezikwa na jeneza hilo aliripotiwa kuzikwa kwa nguo za bei ghali pia.
Wanakijiji walisema kuwa vijana walianza kuiba majeneza eneo hilo kutokana na ukosefu wa ajira.
Wakazi wa kijiji cha Kirichu katika kaunti ya Nyeri waliamka kwa mshangao Alhamisi,Januari 25 walipopata kaburi la mwanamke aliyezikwa hivi majuzi limefukuliwa na jeneza kuwachwa likionekana. Kulingana na wakazi, marehemu alizikwa kwa jeneza la thamani ya Kshs 80,000 na mavazi ya bei ghali.
Wenyeji walishuku kuwa wezi hao walijaribu kuiba jeneza na nguo kutoka kwa mwili wa marehemu.
Wezi hao walichimba kaburi hilo wakijaribu kuondoa jeneza lakini wakakosa kumaliza kazi hiyo machweo ilipotimia. Walipoondoka, walikuwa wamechimba na kufikia jeneza lenyewe, msalaba ukionekana kutoka juu.
Wakazi eneo hilo wamekashifu tukio hilo wakidai kuwa visa vya wizi vimeongezeka eneo hilo, hasa wizi wa majeneza ambao unadaiwa kutekelezwa na vijana ambao hawana ajira
Wakazi waliwaomba vijana eneo hilo kutumia mbinu tofauti kutafuta mapato badala ya kuiba majeneza.:
No comments:
Post a Comment