Bw
Miguna Miguna alijaribu kurejea Kenya Jumatatu lakini akazuiwa kuingia baada
yake kudaiwa kutowasilisha pasipoti ya Canada ambayo ilitumiwa kumsafirisha kwa
nguvu hadi Canada.
Wakili
huyo alisisitiza kwamba ni raia wa Kenya na hafai kuzuiwa kurejea.
Taarifa
zinasema Bw Miguna, ambaye pasipoti yake ya Kenya ilitwaliwa na polisi kabla ya
kuondolewa kwake Kenya mwezi jana, alikuwa ametakiwa kuwasilisha ombi la kupata
visa ya kukaa Kenya kwa miezi sita kwa kutumia pasipoti hiyo yake ya Canada.
Alikataa
jaribio hilo na badala yake kutoa kitambulisho chake cha taifa kuonesha kwamba
yeye ni Mkenya na kutaka aruhusiwe kuingia.
Bw
Miguna, aliyekuwa amewasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta
mwendo wa saa nane adhuhuri, alikesha kwenye uwanja huo.
Maafisa
walijaribu kumsafirisha kutoka uwanja huo kwa kutumia ndege ya shirika la
Emirates ambayo ilikuwa inaelekea Canada kupitia Dubai.
Wakili
wa upinzani James Orengo, seneta ambaye majuzi alichaguliwa kuwa kiongozi wa
upinzani Bunge la Seneti, ameambia Reuters kwamba maafisa wa polisi waliokuwa
wamevalia mavazi ya kiraia ndio waliojaribu kumlazimisha Bw Miguna kupanda
ndege hiyo iliyokuwa inaondoka.
Lakini wakili huyo
alikataa kuingia ndani ya ndege hiyo na mtafaruku ukazuka.
Video
iliyopeperushwa moja kwa moja na runinga ya kibinafsi ya Citizen ilimuonesha Bw
Miguna akiwa kwenye lango la ndege akiwaambia wahudumu: "Siendi popote,
hamuwezi kuniondoa kutoka kwa nchi yangu kwa nguvu."
Bw
Orengo ameambia Reuters kwamba maafisa hao wa polisi baadaye walimuondoa
mwanasiasa huyo kutoka kwenye ndege hiyo na kumzuilia kwa muda katika afisi za
uhamiaji katika uwanja huo wa JKIA.
No comments:
Post a Comment