WAFAHAM MBWA MWITU NA TABIA ZAO ZA KIPEKEE - NIJUZE NEWS

Breaking news

Nyumba ya Habari Makini na za Uhakika

Pata Habari Mpya kwa kina Kila muda kutoka kwanye vyanzo vya Uhakika

Mikoani leo

Mikoani leo

Sunday, February 11, 2018

WAFAHAM MBWA MWITU NA TABIA ZAO ZA KIPEKEE



Image result for PICHA ZA MBWA MWITU


Katika mfululizo wa makala za utalii leo nakuletea makala ihusuyo mnyama ajulikanaye kwa jina la Mbwa Mwatu wa Africa au kwa Kimombo anaitwa WOLVES

 Na mnyama huyu huwezi mpata mnyama huyu nje ya bara la Afrika indio maana akaitwa Mbwa Mwitu wa Africa”

UTANGULIZI
Mbwa mwitu wa Afrika ni wanyama jamii ya mbwa ambao wana sifa kem kem zenye kuvutia hasa wawapo kwenye kundi lao la ujamaa. Ni wanyama ambao wanafahamika sana kwa umoja na ushirikiano hasa pale wanapokuwa kwenye mawindo.

 Lakini wanyama hawa wamekuwa wakikumbwa na changamoto nyingi sana na mpaka kufikia hatua kuwekwa kwenye kundi la wanyama waliyo hatarini kutoweka duniani.

 Lakini ni rahisi kuwa tofautisha mbwa mwitu hawa na jamii nyingine za mbwa mfano mbwa wa nyumbani na wale wengine wa porini.

Basi nikusihi ndugu msomaji wa makala hii kuwa name mwanzo mpaka mwisho wa darasa hili huru kwani utajifunza mambo mengi sana kuhusu wanyama hawa ambao ni fahari ya Afrika lakini pia hapa kwetu Tanzania kwani bado tunao wanyama hawa.

SIFA NA TABIA  ZA MBWA MWITU WA AFRIKA
1.Ni wanyama ambao wanaishi kwa ujamaa na ushirikiano mkubwa sana na inasemekana wapo katika nafasi ya juu sana miongoni wa wanyama wanaoishi kwa ushirikiano.

2.Wana manyoa yenye aina mbali mbali za rangi zenye kuvutina na hasa jinsi zinavoonekana mwilini mwake. 

Rangi hizi mwilini mwa mbwa mwitu wa Afrika ni pamoja na nyekundu, nyeusi, nyeupe, kahawia na njano ambayo kila mnyama mmoja ana mpangilio wa rangi mwilini mwake na kamwe mnyama mmoja na mwingine huwa hawafanani.

3.Rangi za manyoa yao huwa saidia wanyama hawa kujificha katika mazingira wanayo ishi na hivyo kuwa ngumu kuonekana na maadui au wanyama hatarishi kwao.

4.Wana masikio makubwa, pua ndefu, miguu mirefu na vidole vine kwenye kila mguu.

5.Kundi la mbwa mwitu linaweza kuwa na idadi ya wanyama 10-30.

6.Huishi kwa kusaidiana sana hasa pale mwenzao anapo kuwa mgonjw lakini pia husaidiana hata kipindi cha kulea watoto.

7.Mbwa mwitu wa Afrika huwasiliana baina ya mmoja na mwingine kwa kutumia njia mbalimbali mfano kugusana, sauti na mijongeo pia.

8.Kabla ya kuanza kuwinda hujikusanya kwenye kundi moja na kuwa karibu zaidi ili kufanikisha ufanisi katika mawindo yao.

9.Endapo mmoja atatoweka kwenye kundi na kurudi baadae wenzake humuuwa kwani huja na harufu nyingine hivyo hana budi kukimbia nakwenda kuanza maisha mapya.
Je unajua?

1.Mbwa mwitu wana vidole vinne kwenye kila mguu na hii ni moja kati ya tofauti kubwa kati ya wanyama hawa na jamii za wanyama wengine walao nyama?
2.Mbwa mwitu ni miongoni mwa wanyama ambao humla mnyama waliyo muwinda akiwa bado anapumua?

KIMO,  UREFU UZITO  WA MBWA MWITU WA AFRIKA
Kimo= kimo hufikia hadi inchi 30 au zaidi ( takribani sawa na futi 3)
Urefu=hufikia urefu wa inchi 30-56 (sawa na futi 3-5)
Uzito=hufikia uzito mpaka wa kilogramu 18kg – 25kg

MAZINGIRA
Mbwa mwitu ni wanyama ambao wana uwezo wa kuishi katika mazingira mbali mbali mfano maeneo yenye majani, jangwa na misitu.

CHAKULA
Mbwa mwitu ni miongoni mwa jamii ya wanyama walao nyama na hupendelea sana kuwinda wanyama wa maumbo ya kati kama swala pala, pongo, swala tomi na ngiri.

KUZALIANA
Mara tu baada ya kupandana mbwa mwitu jike hukaa na mimba kwa takribani siku 70 (sawa na miezi miwili na siku kumi).

 Kisha huzaa kuanzia watoto wawili hadi ishirini (watoto 2-20) na kubaki anawachunga ndani ya wiki chache mpaka watakapoweza kujitegemea. Huwa tegemea wenzake ndani ya kundi kwa ajili ya chakula.

Watoto wa mbwa mwitu wa Arika huanza kujichanganya kwenye kundi baada ya miezi miwili mpaka mitatu baada ya kuzaliwa na wakati huu husaidiwa na kundi zima katika suala la chakula la ulinzi pia mpaka pale watakapo kuwa na uwezo wa kujitegemea wenyewe na hapa ndipo huondoka nakujiunga na makundi mengine au kuanzisha kundi lao wenyewe. 

Na inasemekana kadri wanavyo zidi kuwachunga watoto ndo uwezekano wa watoto hao kukua unaongezeka.

Maisha ya mbwa mwitu wa Afrika awapo katika maeneo yake ya asili hufikia miaka kumi hadi kumi na mbili ( miaka 10 – 12).

UHIFADHI NA IDADI YA MBWA MWITU 
Kutokana na takwimu za shirika la umoja wa mataifa linalo shughulika na uhifadhi wa maumbile asili ( International Union for Conservation of Nature – IUCN), mbwa mwitu wa Afrika ni wanyama waliyo hatarini kutoweka duniani.

 Kama nilivo dokeza hapo juu wanyama hawa hawapatikani sehemu nyingine yoyote duniani zaidi ya bara la Afrika na ni nchi chache tu pia humu barani Afrika utaweza kuwaona wanyama hawa.

Wanyama hawa wamekuwa wakilindwa sana ili wasitoweke hususani hapa nchini kwetu Tanzania lakini bado kuna wasiwasi juu ya kuongezeka kwa wanyama hawa nah ii ni kutokana na msukumo mdogo wa uchangiaji wa uhifadhi wa wanyama hawa. 


Image result for PICHA ZA MBWA MWITU
Lakini utafiti umebaini kuwa idadi ya wanyama hawa inapungua siku baada ya siku.

Takwimu zinaonyesha kwa sasa idadi ya Mbwa mwitu wa Afrika katika bara zima la Afrika haizidi wanyama 7,000. 
Hii inaskitisha sana kwani ni idadi ndogo sana hii tukilinganisha na wanyamapori wengine.

UHIFADHI NA IDADI YA MBWA MWITU 
Kutokana na takwimu za shirika la umoja wa mataifa linalo shughulika na uhifadhi wa maumbile asili ( International Union for Conservation of Nature – IUCN), mbwa mwitu wa Afrika ni wanyama waliyo hatarini kutoweka duniani. 


Image result for PICHA ZA MBWA MWITU

Kama nilivo dokeza hapo juu wanyama hawa hawapatikani sehemu nyingine yoyote duniani zaidi ya bara la Afrika na ni nchi chache tu pia humu barani Afrika utaweza kuwaona wanyama hawa.

Wanyama hawa wamekuwa wakilindwa sana ili wasitoweke hususani hapa nchini kwetu Tanzania lakini bado kuna wasiwasi juu ya kuongezeka kwa wanyama hawa nah ii ni kutokana na msukumo mdogo wa uchangiaji wa uhifadhi wa wanyama hawa.

 Lakini utafiti umebaini kuwa idadi ya wanyama hawa inapungua siku baada ya siku.
Takwimu zinaonyesha kwa sasa idadi ya Mbwa mwitu wa Afrika katika bara zima la Afrika haizidi wanyama 7,000. 

Hii inaskitisha sana kwani ni idadi ndogo sana hii tukilinganisha na wanyamapori wengine.

TISHIO  NA MAADUI  KWA MBWA MWITU WA AFRIKA HASA HAPA KWETU TANZANIA
1.Tishio kubwa sana kwa mbwa mwitu wa Afrika ni wafugaji ambao wamekuwa wakiwauwa wanyama hawa kwa hofu ya kuliwa mifugo yao.


Image result for what is wolve

 Wafugaji wamekuwa wakiuwa wanyama hawa kwa kasi kubwa hatimae kupelekea wanyama hawa kuwa hatarinikutoweka.

2.Magonjwa, haya pia ni changamoto au tishio la pili kwa wanyama hawa na hii ni kutokana na uharibifu wa mazingira ambao pia unapelekea muingiliano baina ya mbwa mwitu wa Afrika na binaadamu hali kadhalika wanyama wafugwao majumbani.

3.Uharibifu wa mazingira na uzibaji wa maeneo wanayo tembelea wanyama hawa kwani imepelekea wanyama hawa kubaki na eneo dogo sana la kuzungukia. 

Hii imepelekea kushindwa kuenea maeneo mengi kwani myanya ya mizunguko yao kwa sasa imezibwa hasa kutokana na uharibifu wa mazingira na shughuli za kibinaadamu.

4.Kuna maadui kama fisi na simba ambao pia wamekuwa wakiwasumbua mbwa mwitu wa Afrika japo hii hutokea endapo simba au fisi wata mkuta mbwa mwitu huyo akiwa peke yake na sio kwenye kundi. 

Kwani mbwa mwitu wawapo kwenye kundi huwa hawana uoga na ni majasiri sana kiasi kwamba wana uwezo wa kumuuwa hata simba.

NINI KIFANYIKE KUWANUSURU MBWA MWITU WA AFRIKA HUSUSANI HAPA KWETU TANZANIA
1.Kuhakikisha maeneo yaliyopo yana hifadhiwa vizuri lakini pia kuongeza maeneo ambayo yata ruhusu mbwa mwitu kutembea eneo kubwa na kuunganisha maeneo ya mapitio ya wanyama hawa ambayo yamezibwa kwani yataongeza hata uwezekano wa kuzaliana kwa wanyama hawa.

2.Mamlaka husika zihakikishe zinafanya kazi ja jamii zinazo zunguka maeneo ya hifadhi na hata jamii ambazo zipo mbali ili kupunguza au kuepuka kabisa suala la mauwaji ya wanyama hawa kutokana na migogoro inayo endelea baina ya wanyamapori  na binaadamu.

3.Kuanzisha mbinu mbali mbali ambazo zitasaidia kulinda makundi madogo madogo ya mbwa mwitu hasa kutokana na magonjwa ambayo yanaonekana kuwa tishio la pili kwa wanyama hawa.

4.Zifanyike tafiti za mara kwa mara ili kugundua maeneo yanayo athirika zaidi na uharibifu wa mazingira na kuathiri ongezeko la wanyama hawa ili kutanua uga kwa ajili ya mtawanyoko na kuzaliana kwa mbwa mwitu hawa.

5.Ufuatiliaji wa mara kwa mara wa uelekeo wa wanyama hawa lakini pia kujua baadhi ya magonjwa mengine yanayo zuka huenda yakaja kuwa tishio kubwa sana na kupunguza kasi ya kuongezeka kwa wanyama hawa.
  1. Jamii za wafugaji zinazoishi karibu na maeneo ya hifadhi za taifa zitafutiwe maeneo mengine yenye aridhi nzuri inayo ruhusu majani kwa ajili ya mifugo yao ili kupunguza au kutokomeza adha ya kuuwawa kwa wanyama hawa kwa kile kisemwachokama kulipa kisasi kutokana na kuliwa kwa mifugo yao7.Serikali kupitia wizara ya maliasili na utalii pamoja na mamlaka za uhifadhi wanyamapori kwapamoja wasaidiane kuanzisha maeneo maalumu kwaajili ya kuwafuga wanyama hawa waweze kuzaliana ili kuongeza idadi yao na kasha kuwaachia hifadhini.

HITIMISHO
Wanyama hawa wamekuwa wakipungua kwa kasii kubwa sana na kusababisha mgongano mkubwa sana katika vichwa vya watu hasa wale wathaminio uhifadhi wa wanyamapori. Kuna wakati idara za hifadhi ya taifa ya Serengeti walijitahidi sana kuwatunza wanyama hawa na kuwazalisha ili idadi iweze kuongezeka na shukrani walifanikiwa kwa hilo.
 Lakini kwa sasa na takwimu zinaonesha kuwa idadi ya wanyama hawa bado inazidi kupungua sana na kwa hakika inahitajika jitihada kubwa sana ili kuwanusuru wanyama hawa.

Nasi wananchi tujitahidi kutoa ushirikiano ili kunusuru wanyama hawa tuendelee kuwa nao kw vizazi vya sasa na vijavyo.

Maoni, ushauri.: Call/ sms.whatsaap +255764228384

No comments:

Post a Comment

Mikoani leo

Mikoani leo