Siku zinayoyoma na sasa ni mwezi wa kwanza(1)
mjasiriamli jiulize umefanya nini mpaka sasa?
Ni yapi yalikuwa malengo yako kwa mwaka
huu katika biashara na je, umefanikiwa kiasi
gani mpaka sasa na zipi zimekuwa
changamoto na umekabiliana nazo vipi?
Nawashukuru wote
Mnaonipa mrejesho juu ya mada mbali mbali ninazozitoa.
Leo katika kona ya wajasiriamali tutaona
moja ya siri inayoweza kujenga mafanikio
katika ujasiriamali, nayo ni nguvu iliyopo
katika uvumilivu.
Uvumilivu ni nini?
Uvumilivu ni hali ya kukubali
na kukabili jambo kadiri ya wakati na jinsi
linavyotokea.
Kumbuka kuwa mafanikio katika biashara si
jambo la kulala na kuamka, bali ni suala
linalohitaji uvumilivu wa kweli. Hivyo kwa
wale wajasiriamali wenye kiu ya mafanikio
wanahitaji kuzingatia mbinu za ujasiriamali
katika uvumilivu ili kupata mafanikio.
Hebu jiulize una malengo gani
katika ujasiriamali? Siri kubwa ya kufanikiwa
ni kujiwekea malengo. Malengo ni ndoto za
kweli juu ya mambo unayotaka uyapate,
kwamba katika kipindi cha muda fulani uwe
umeweza kufanya jambo fulani.
Katika malengo ni muhimu kuwa na uvumilivu,
si kila unalopanga litakuja kama unavyotaka.
Elewa katika malengo yako huenda ukakutana
na changamoto mbalimbali zinazoweza
kukwamisha yale uliyoyapanga na hivyo
kurudi nyuma.
Kumbuka mjasiriamali ni vizuri kujiwekea
malengo ambayo unaweza kuyafikia na si
kujifurahisha. Ndio maana tunasema unahitaji
kuwa mvumilivu, usikurupuke kwa kuwa tu
umeona mwenzio anafanya jambo fulani na
wewe unataka kufuata mkumbo.
Wajasiriamali wote ambao wamefanikiwa
walianza na mawazo madogo yaliyowapeleka
kwenye mawazo makubwa. Mafanikio katika
ujasiriamali hayaji kama upepo bali lazima
udhamirie na kuanza harakati za kuelekea
unakotaka.
Yafaa kujiuliza kwanini unafanya biashara
unayofanya, ni kitu gani kilikusukuma uingie
katika biashara hiyo na si nyinginezo? Sababu
ya wewe kufanya unachofanya kwa sasa ni
ufunguo wa mafanikio.
Wengi wameingia kwenye ujasiriamali kwaajili
ya kutafuta mafanikio, na kilele cha mafanikio
ni hupimwa kwa fedha na mali wanazopta, je,
umewahi kujiuliza ni kiasi gani cha kipato au
mali unahitaji kumiliki na utapataje?
Umewahi kujiuliza kwanini baadhi ya
wajasiriamali wanashindwa kufikia ndoto zao?
Umeshawahi kujiuliza kwanini kuna
wajasiriamali waliofanikiwa na ambao
hawajafanikiwa? Hawa waliofanikiwa
wamewezaje kufika huko?
Amka ndugu mjasiriamali, malengo ni silaha
ya kukupeleka kule unakotaka. Acha kufanya
mambo kimazoea kwa kuwa tu unapata hela
ya kula na kulipa ada, elewa kuwa malengo
yenye kufaa yanaweza kukupeleka mbali zaidi.
Pamoja na kujiwekea malengo, ni muhimu
sana tena sana kufanyia kazi yale unayotaka
kuyafikia. Wapo ambao wana mipango mizuri
vichwani, lakini katika utekelezaji wake huwa
ni mzigo kwao, maneno na matendo yao
hayawiani!
Ili ufanikiwe unahitaji kuamka na kutafuta
namna ya kuweza kutekeleza yale yote
uliyojipangia. Kujiwekea malengo yoyote bila
kutafuta namna ya kuyafikia ni sawa na bure.
Kaa chini uumize kichwa ni kwa namna gani
utaweza kufikia malengo yako
No comments:
Post a Comment