FURSA: BIASHARA YA HOTEL/RESTAURANT - NIJUZE NEWS

Breaking news

Nyumba ya Habari Makini na za Uhakika

Pata Habari Mpya kwa kina Kila muda kutoka kwanye vyanzo vya Uhakika

Mikoani leo

Mikoani leo

Thursday, January 18, 2018

FURSA: BIASHARA YA HOTEL/RESTAURANT


Mahitaji:

Viti vya kuvutia,Meza Nzuri Za
Pembe nne Au duara ni nzurii,Vitambaa vya
mezani ( Vyekundu Au Blurish ) ,Maua mazuri
ya kuweke mezani na mapambo kadhaa ili
mradi meza isijazwe,Pazia za Mlangoni
Nyeupe zitafaa, Masufuria ya kupikia, Sahani
nzuri na za kuwavutia wateja,Vijiko simple
vyenye mahadhi tofauti,Wafanyakazi unaweza
kuanza na wanne 2 jikoni 2 huduma.Biashara
inavyokuwa unazidi kuongeza ,Picha nzuri za
kuvutia za kuweke ukutani,Miavuli nje ya
kupumzikia ,Maua kwa Nje yasiyo asili au
pandikizwa,Bulb za rangi kwa nje wakati wa
usiku.,Sare za wafanyakazi ,tshirts nyeupe na
nyeusi(black) suruali or sketi au tshirts red na
sketi nyeupe ,Kapeti ya chini inayovutia,kochi
au sofa la kupumzikia wateja,Kabati ya kioo
kwa ajili ya kuwekea vitafunwa na chakula,
Maji ya kunawia ya vuguvugu yatafaa
sana,Meza ya mpokeaji pesa, sio kila mtu awe
mpokee pesa.,Vitambaa vyeupe vya kufutia
Meza,Feni,Tv / Radio .Nakadhalika.


Aina za vyakula vinavyowavutia wateja.

1.Wali
2.Nyama
3.Samaki
4.Dagaa
5.Mboga za majani.
6 .Maharage.
7.Ugali
8.Ndizi
9.Supu, Mbuzi, Ngombe, Kuku.
10.Chipsi za kisasa zenye mchanganyiko
mwingi.
11.Chai ,Maziwa, Maziwa fresh, Rangi.N.k
12.Juice, Soda, N.k
13.Vitafunywa kama Chapati, Maandazi,
Cakes,Maandazi marefu, Viazi,
Karanga,Donatis.
Lakini kabla hujafungua mradi wako inatakiwa
ufanye utafiti wa eneo kwa muda wa Miezi
3-6 kitaalamu ili ujue wateja nini wanapenda
na mambo mengine kama huduma gani
nyingine hoteli za jirani hazitoi ili uje na
Mpango madhubuti,Uwajue wateja wako ni
wakubwa Au watoto, ni wa kipato gani N.k


Mahali pazuri pa kufanyia biashara ya
hoteli Au restaurant.
1.Maeno ya wanafunzi( primary,seconda
ry,collegs, Universities.
2.Maeneo yaliyokaribu na ofisi nyingi mfano
posta, bomani N.k
3.Maeneo yanayopakana na hospitali.
Maeneo ya stendi na vituo vya magari.
4.Maeneo ya makutano ya watu.
5.Maeneo ya Mijini
6.Maeneo ya watu wanapofanyia miradi
mfano ujenzi wa miradi mbalimbali.
7.Vituoni. Vya magari,pikipiki nk.
8.Maeneo ya Makanisa ya mikutano ya Mara
kwa mara.
9.Maeneo ya kambi mbalimbali za mafunzo.
Kwa Ujumla Maeneo yenye umati mwingi.

Kipi ni bora bei Au thamani na ubora wa
chakula, vyote hivi ni bora kwa mteja lakini
quality ya chakula ni nzurii sana kama
unauzia watu wa hadhi Fulani,
Pia unapopanga bei zingatia gharama zako
( cost oriented pricing approach ),Angalia pia
bei za washindani wako sokoni ( competitors
based pricing) Au Market oriented pricing.
Unapoanza unaweza kuwavuta wateja wako
kwa kuanza kuuza kwa bei ya chini
( penetration method )Au bei ya juu
( skimming method) lakini wengi hutumia low
prices market entry strategy.


Njia za kuwashinda washindani wako.
1.Toa ofaa kama pipi Au jojo baada ya
huduma.
2.Weka chai ya bure wakati wa jioni, njia hii
iliwahi kutumika na chuo Cha Dsm Mabibo
hostel cafeteria na wanafunzi wengi walienda
kwa ajili ya chai.
3.Chemsha maji ya kunywa na toa bure kwa
muda wa miezi kadhaa ili kupata wateja
wengi.
4.Madhari ya hoteli yako yavutie sana.
5.Weka television Au mziki ,kuna wateja
hupenda kula sehemu yenye mziki na Tv.
6.Weka huduma za ziada kama Mpesa kwenye
Meza ya kupokelea malipo.
7.Mteja akileta mteja mwingine apewe chai ya
maziwa Au chapati 1 bure.
8.Tumia lugha nzurii na ya ukarimu sana.
9.Tengenza fliers Na posters zinazolezea
biashara yako.
10.Weka Bango nje la hoteli yako.
11.Tengeneza sare zenye nembo ya hoteli
yako.
12.Chakula Au huduma baadhi ziwe katika
packages Mfano Chips Mayai.
13.Maintain usafi wa mazingira ya eneo lako
la hoteli ,through out the day asubuhi mpaka
jioni.
14.Mteja hakoseagi hivyo epuka kulumbana
na Mteja kwani kufanya hivyo kutasababisha
akuhame.
14.Na Kama ni hoteli kubwa tangaza radioni,
Tv,Magazeti,Blogs N.k
Asanteni Sana

Endelea kujifunza mengi

No comments:

Post a Comment

Mikoani leo

Mikoani leo