Hili ni la muhimu kwa
kuwa ndilo linalokufanya upatenguvu za kufikia ndoto zako
ama ufeli kabisa.
Tumetofautiana;wengine tafsiri
ya wao ni nani huipata kutokana
na maoni ya watu
wanaowazunguka,wengine ni
kutoka na hali walizopitia huko
nyuma(kama walifeli au
kushindwa basi wanajiona ni
watu wasioweza kufanikiwa) na
wengine hujitafsiri kulingana na
walichoambiwa na wazazi wao.
Jambo la muhimu ni kuwa tafsiri
yako binafsi ina nguvu kuliko
tafsiri ya mtu mwingine
yeyote:”Ajionavyo mtu nafsini
mwake(ndani ya moyo wake)
ndivyo alivyo”-Mithali 23:7.
Utafiti wa kisaikolojia
unaonyesha kuwa watu wengi
huvaa,huongea na hata
kuhusiana na wengine kulingana
na picha wanayoiona ndani yao
kuhusu wao ni nani.Ndio maana
watu ambao wameshajiona
washindi huwa hawakubali
kushindwa hata iweje lakini watu
ambao wameshajiona
hawatafanikiwa huwa kitu kidogo
kikitokea wanakata tamaa.
Hatima ya maisha yako iko
kwenye picha unayoibeba
moyoni mwako na sio mambo
yanayokuzunguka,yaliyokutokea
au watu wanasema nini kuhusu
wewe…UNAVYOJIONA NDIVYO
UTAKAVYOKUWA.Kanuni hii ina
nguvu sana ndio maana
walipomwambia walter Disney
hana “imagination” yeye alijiona
anayo na leo utajiri wake bado
unaendelea.
Ndio maana walipomwambia
Mandela hatainuka tena
aliendelea kujiona ni Rais wa
Afrika Kusini hata akiwa
gerezani na baada ya miaka 27
kifungoni ndoto yake ilitimia.Bila
kujali itachukua muda gani
ilimradi hautapoteza ndoto yako
moyoni mwako ipo siku itatimia.
Je,unajionaje?Bila kujali hali
uliyonayo kwa sasa,bila kujali
watu wanakuonaje kwa sasa au
wanasema nini kuhusu
wewe..Endelea kushikilia picha
unayotaka ya maisha yako na
utafikia hatima yako.Nguvu ya
Kubadilisha hali uliyonayo
inatokana na picha uliyoibeba
kuhusu kesho yako;Bila Kujali
Changamoto za Leo
No comments:
Post a Comment