Meya wa Dar es Salaam, Bw. Iyasa Mwita (Picha ya Mtandao) |
Bw. Mwita ameyasema hayo leo January 20, mwaka huu wakati akirishiri kuchimba mtaro na wakazi wa mtaa wa Kidongoni kata ya Vijibweni Wilaya ya Kigamboni, jijini Dar es Salaam
Mwita ambeya pia ni diwani wa Kata ya Vijibweni amesema kuwa wakati wa enzi za Rais wa awamu ya kwanza ya Hayati Mwl Julius Kambarage Nyerere watu walikuwa wanalijingewa dhana ya kujitegemea kupitia vijiji vya Ujamaa.
"Enzi za Mwalimu (hayati baba wa Taifa Julius Nyerere) miaka ya 1970 aliunda sera ya Ujamaa na kuunda vijiji vya ujamaa, hii ilikuwa kushiriki shughuli za maendeleo hivyo na sisi hatuna budu kufanya kazi kwa bidii. Alisema Meya.
aliongeza kuwa tofauti ya vyama isitufanye tusishiriki shughuli za Maendeleo
" Nmeshamwambia Rais Magufuli kuwa wewe una chama chako na mimi nina chama changu lakini kwenye maendeleo ni lazima tushirkiane " ameongeza Mwita huku wakazi walioshiriki wakaimushangilia.
Meya Mwita pia amewata wajumbe wa nyumba kumi kutoa taarifa za changamoto zinazowakumba wananchi ili aweze kuzitaitua.
Mtaro huo wenye urefu wa takribani kilomita 2 ulijengwa tangu enzi ukoloni na kufunikwa na undongo umekuwa kero kwa wakazi eneo hilo na kusababisha maji kujaa.
No comments:
Post a Comment