Rais wa Marekani, Donald Trump |
Hatua hiyo imesbabisha huduma nyingi za serikali kukwama lakini, hata hivyo athari kamili
itaanza kuonekana siku ya Jumatatu, wakati wafanyakazi wa serikali watarejea
kazini.
Mara ya mwisho
shughuli za serikali zilikwama nchini Marekani ni mwaka wa elfu mbili na kumi
na tatu, na ilidumu kwa muda wa siku kumi na sita wakati ambapo wafanyakazi
wengi wa serikali walishurutishwa kwenda likizo ya lazima.
Ni mara ya kwanza
kwa huduma za serikali kukwama huku chama cha Republican kiki dhibiti mabunge yote
na ikulu ya White house.
Wabunge wa Bunge la Seneti |
Ikulu ya White House
imewalaumu wabunge wa chama cha Democrats kwa kuweka siasa juu ya maswala ya kiusalama ,
familia za wanajeshi, watoto walio katika mazingira magumu, na uwezo wa taifa
hilo kuwahudumia raia wa Marekani
Hata hivyo
atakayeshindwa katika mkwamo huu ni chama kitakachoingia katika vita na idadi
ndogo ya wabunge ikiwa ni habari mbaya kwa rais Trump na chama cha Republicans.
Habari
njema ni kwamba , pande zote mbili na ngome zao za kisiasa zitafurahishwa kwa
kufanya mambo kuwa magumu.
Suala linalogombaniwa ni lile la Democrats kutaka zaidi ya wahamiaji wasio na vibali
walioingia nchini Marekani kutofurushwa.
Wahamiaji
hao walipatiwa vibali vya kuwa nchini humo kwa muda chini ya mradi ulioanzishwa
na rais wa zamani Barrack Obama.
Mnamo mwezi
Septemba, Rais Trump alitanngaza kushitisha mpango huo huku akilipatia
bunge la Congress hadi mwezi Machi kuwa na mpango mbadala.
No comments:
Post a Comment