ZIJUE TOFAUTI KATI YA KAZI" NA "AJIRA", soma hapa kujua to tofauti ya neno kazi na neno ajira - NIJUZE NEWS

Breaking news

Nyumba ya Habari Makini na za Uhakika

Pata Habari Mpya kwa kina Kila muda kutoka kwanye vyanzo vya Uhakika

Mikoani leo

Mikoani leo

Thursday, January 18, 2018

ZIJUE TOFAUTI KATI YA KAZI" NA "AJIRA", soma hapa kujua to tofauti ya neno kazi na neno ajira

14316853_164718120637143_4579398951985275579_n
“Ajira” ni kufanya kazi ambayo siyo ya
kwako, waweza kuwa unaipenda au
huipendi. Watu wengine hawapendi kazi
walizoajiriwa kuzifanya, lakini
yawezekana wanaendelea kufanya kazi
hizo kwasababu wanalipwa pesa.
Kutokana na hali hii, watu wengi
hulazimika kutafuta kazi nyingine pale tu
malipo yanapokuwa hayatoshelezi mahitaji
ya muhusika. Mwenye kazi “mwajiri”
anapokuwa amekuajiri kwenye kazi yake
ambayo “ siyo ya kwako”; wewe moja kwa
moja unahesabika kuwa ni sehemu ya
gharama za uendeshaji wa kazi au
kampuni! Hii ni sawa na kusema kuwa
waajiri wengi wanawaona wafanyakazi
(waajiriwa) kama gharama za uzalishaji!.
Hii haina maana kwamba waajiri
hawawathamini waajiriwa wao, bali
wakati wa kufanya tathimini ya maendeleo
ya kazi inawabidi kufanya hivyo, ili
kupanga mipango mikakati ya kuwezesha
matunda ya kazi husika yapatikane kwa
gharama nafuu.
“Kazi” ni majumuisho ya majukumu
mbalimbali ambayo kwa mwenye kazi
unajiwajibisha mwenyewe katika
kuyatimiza hayo uliyojipa mwenyewe, bila
kutegemea kulipwa chochote mpaka
matunda ya kazi hiyo yapatikane.
Unapofanya kazi siyo lazima alipwe,
kwasababu mara nyingi kazi inakuwa ni
mchakato wako wa maisha na haupangiwi
na mtu yeyote, wewe mwenyewe
unajipangia ni nini ufanye, kwa malengo
yapi na ni nani unamlenga kunufaika na
matokeo (matunda) ya kazi yako. Iwapo
matokeo ya kazi yako yanatoa suluhisho la
matatizo au kero zilizopo kwenye jamii
husika, basi ujiandae kulipwa malipo
ambayo hayana kikomo, kwasababu watu
watanunua matunda ya kazi yako, ili
kukidhi mahitaji yao, hivyo ni rahisi wewe
kuweza kutajirika kutajirika kupitia
utatuzi wa kero na matatizo mbalimbali.

No comments:

Post a Comment

Mikoani leo