Hivi za hivi karibuni, kumekuwa na malalamiko, kutoelewana kwa
wanandoa wengi kiasi cha kupelekea mahusiano na ndoa za kusambaratika, sabubabu
kuu ikielezwa kuwa ni upungufu wa nguvu za kiume
Upungufu wa nguvu za kiume Maana yake Nini?
Upungufu
wa nguvu za kiume ni hali ya kiungo cha uzazi cha mwanaume
(uume) kutokuwa na nguvu ya kutosha kufanikisha tendo la ndoa kama vile
kushindwa kuanza au kukamilisha tendo lenyewe.
Vilevile nguvu za kiume huanza kupungua kuanzia umri wa miaka
50.
Mabadiliko haya ni ya
kawaida, hayahusiani na tatizo lolote la kiafya endapo hayasababishi kushindwa
kabisa tendo la ndoa.
Ili uume uweze kuwa na nguvu ya kufanikisha tendo la ndoa ni
lazima damu iende kwenye mishipa ya uume kwa kiwango cha kutosha na iweze
kubaki sehemu hiyo kwa muda mrefu.
Sehemu mbalimbali za mwili zinafanya kazi kwa pamoja kuhakikisha
mfumo huu mzima unafanya kazi sawasawa ikiwa ni pamoja na mishipa ya damu na
fahamu, ubongo pamoja na vichocheo vya mwili (hormones).
Hali yoyote ya mwili inayosababisha damu kushindwa kufika kwenye
mishipa ya uume au kutokaa muda wa kutosha, na hitilafu katika mfumo wa neva
kati ya uume na ubongo inaweza kuleta upungufu wa nguvu za kiume.
Vile vile saikolojia ina sehemu kubwa katika kufanikisha tendo
la ndoa. Sababu za kupungua kwa nguvu za kiume zimegawanyika katika makundi
makuu mawili; sababu za kiafya na sababu za kisaikolojia.
Matatizo ya kiafya ambayo yanasababisha upungufu wa nguvu za
kiume ni magonjwa ya moyo, kisukari na shinikizo la juu la damu; uzito mkubwa;
na baadhi ya dawa. Mfumo wa maisha unaoongeza uwezekano wa kupunguza nguvu za
kiume ni unywaji wa pombe kupita kiasi na uvutaji sigara.
Sababu za kisaikolojia ni pamoja na hali ya wasiwasi, msongo wa
mawazo au kutokuwa na maelewano na mwenza wako. Mara nyingi sababu za kiafya na
kisaikolojia hutokea kwa pamoja na zinategemeana; hasa kwa sababu kukosekana
kwa nguvu za kiume kunaleta athari za saikolojia; athari za kisaikolojia
zinaleta upungufu wa nguvu za kiume; hivyo kunakuwa na mzunguko wa tatizo.
Dalili kuu ya upungufu wa
nguvu za kiume ni uume kutokuwa na nguvu ya kutosha
kuanza tendo la ndoa au nguvu kuisha kabla ya kukamilisha tendo. Kupungua kwa
nguvu za kiume kwa sababu za kiafya kunaweza kutofautishwa na sababu za
kisaikolojia kwa kuangalia iwapo kupungua huku ni kwa mfululizo au hutokea kwa
nyakati fulani tu.
Endapo tatizo linatokea kwa nyakati maalumu tu kwa mfano wakati
umebadilisha mwenza, uwezekano mkubwa ni tatizo la kisaikolojia.
Lakini kama tatizo ni la muendelezo na linaongezeka ukubwa siku
hadi siku, inawezekana kuna tatizo la kiafya.
Mtaalamu wa afya anaweza kupambanua na kufanya vipimo
vinavyostahili ili kuweza kubaini chanzo cha tatizo
. Mara nyingi watu wameshindwa kutafuta ushauri wa kitaalamu kwa
wakati, kwa sababu ya kuona kuwa suala hili ni la usiri na wasingependa
kuliongelea; hata hivyo ni muhimu kupata ushauri ili kubaini chanzo na kuweza
kupata msaada wa kitaalamu mapema.
Madhara yatokanayo na upungufu wa guvu za kiume yanaonekana
zaidi katika saikolojia ambapo muathirika anapata msongo wa mawazo na wasiwasi;
vilevile husababisha mafarakano kwenye mahusiano.
Na endapo tatizo ni kubwa linaweza kuleta ugumba. Matibabu ya
upungufu wa nguvu za kiume yanategemea na chanzo cha tatizo
. Iwapo chanzo kitagundulika mfano kama ni dawa za ugonjwa
fulani, daktari anaweza kushauri kubadilisha aina ya dawa; na ikiwa tatizo lipo
kwenye upungufu wa vichocheo vya kiume daktari anaweza kushauri kutumia dawa za
kuongeza vichocheo hivyo mwilini.
Vilevile zipo dawa zinazotumika kuongeza msukumo wa damu kwenye
uume na hizi zinatumika ili kuongeza nguvu za kiume.
Japokuwa dawa hizi zinauzwa kwenye maduka ya dawa, ni vizuri
kupata ushauri wa daktari kabla ya kuzitumia ili kuweza kubaini chanzo, na
endapo unastahili kutumia dawa hizo au la.
Njia za kupunguza
uwezekano wa kupata tatizo la kupungua kwa nguvu za kiume ni kuzingatia lishe
bora, kufanya mazoezi, kupunguza unywaji wa pombe na kuacha kuvuta sigara.
Vilevile ni muhimu kupata ushauri wa kitaalamu iwapo unasumbuliwa
na msongo wa mawazo au tatizo lolote la kisaikolojia. Uchunguzi wa afya mara
kwa mara utabainisha magonjwa kama vile kisukari na shinikizo la damu na
kuyadhibiti mapema kabla hayajaleta athari za kupungua kwa nguvu za kiume.
No comments:
Post a Comment