MAUAJI YA KINYAMA YAENDELEA KULITESA TAIFA - NIJUZE NEWS

Breaking news

Nyumba ya Habari Makini na za Uhakika

Pata Habari Mpya kwa kina Kila muda kutoka kwanye vyanzo vya Uhakika

Mikoani leo

Mikoani leo

Tuesday, March 20, 2018

MAUAJI YA KINYAMA YAENDELEA KULITESA TAIFA



FB_IMG_1521542969131.jpg
mabaki ya mifupa yaliopatokana kwenye shimo la mbuyu.
Jeshi la Polisi Mkuoni Singida linamshikilia Bw.a Benard Shumba mkazi wa Singida tuhuma za mauaji ya  mke wake miaka nane iliyopita kisha kuuficha mwili huo kwenye kwenye shimo la mtu mkubwa aina ya mbuyu zaidi.
FB_IMG_1521542979148.jpg

Baada  ya kuhojiwa na Polisi mtuhumiwa amekiri kuteda kosa hilo.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Singida ,Deborah Magiligimba amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, na kusema mtuhumiwa baada ya kukamatwa alikiri kutenda kosa hilo na kwenda kuonesha mwili wa marehemu aliokuwa ameuhifadhi ndani ya mbuyu


Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na wananchi limefanikiwa kupata mabaki ya mwili wa mwanamke huyo yaliyotokea zaidi takribani miaka saba iliopita.
FB_IMG_1521542973582.jpg
“Ni kwamba mnamo tarehe 7/10/2010 huko katika kijiji cha Yulansoni kata na tarafa ya Kinyangiri wilaya ya Mkalama Mkoa wa Singida. Tabu Robert,mnyiramba,28yrs mkulima wa Yulansoni aliuawa na mume wake aitwae Bernard Shumba@Siza,mnyiramba,47yrs,mkulima wa Yulansoni.”


Baada ya Mtuhumiwa kufanya tukio hilo aliuchukua mwili wa marehemu na kwenda kuuficha kwenye mti wa mbuyu ambao unatundu kubwa na kisha aliripoti polisi kituo kidogo cha Kinampanda Mkalama kuwa mke wake ametoroka na alianza kumtafuta hadi tarehe 17/3/2018 taarifa zilipopatikana kuwa alimuua.

Baada ya Mtuhumiwa kukamatwa na kuhojiwa alikiri kufanya tukio hilo nakuonyesha sehemu alipomtupia.tarehe 18/3/3018 saa 16:00hrs OC CID Mkalama na timu yake ya makachero walifika eneo la tukio nakufanikiwa kupata mabaki ya mifupa yakiwa ndani ya mti huo.


Baadhi ya mifupa imechukuliwa kwa ajili yakupeleka kwa mkemia wa serikali na iliyobakia ndugu wamekabidhiwa kwa ajili ya mazishi.
mbuyu.jpg

No comments:

Post a Comment

Mikoani leo

Mikoani leo