Jacob Zuma, Rais wa Afrika Kusini |
Haijafichuliwa
mazungumzo hayo yalihusu nini lakini viongozi katika chama hicho wanatarajiwa
kufanya mkutano wa dharura hii leo Jumatatu.
Cyril
Ramaphosa aliichukuwa nafasi ya kiongozi wa chama cha ANC kutoka kwa Zuma,
anayekabiliwa na tuhuma za rushwa.
Wachambuzi
wanasema wakuu wa chama hicho wanajaribu kuondoa mvutano wa kung'ang'ania
madaraka ambao unaweza kukigawanya chama hicho kabla ya uchaguzi mkuu mwakani.
Wanatarajiwa
kuanza mchakato wa kumuondoa rais Zuma kupitia mfumo rasmi wa kumuondoa au kwa
kuidhinisha hoja bungeni.
Maafisa
sita wakuu wa chama hicho tawala waliwasili mmoja baada ya mwingine Jumapili
katika makaazi ya Zuma mjini Pretoria.
Walinyamaza
kimya wakati mazungumzo yalipomalizika lakini wameitisha mkutano wa kamati kuu
ya chama hicho Jumatatu.
Julius
Malema, kiongozi wa upinzani na aliyekuwa mafuasi wa chama hicho cha ANC
alisema kwenye mtandao wake wa Twitter kwamba rais Zuma amekataa kujiuzulu.
Zuma
anastahili kusalia madarakani hadi uchaguzi mwaka ujao 2019. Hatahivyo chama
hicho kimepoteza umaarufu wake katika muhula wa pili wa kiongozi huyo huku
kukishuhudiwa pia kudorora kwa uchumi na tuhuma za rushwa.
Mustakabali wa
Zuma ni upi?
Rais Zuma anakabiliwa na
tuhuma za rushwa na jitihada za wapinzani na baadhi ya wafuasi wa ANC wanaotaka
kumtimua madarakani.
Kwa mujibu wa taarifa
rasmi, maafisa wa ngazi ya juu wa ANC wana 'jadiliana tu' na rais Zuma kuhusu
"ugavi wa uongozi" ndani ya chama.
Lakini nyuma ya kauli hiyo
nyepesi - vita vikali vya uongozi vinajitokeza katika nchi hiyo.
Rais Zuma bado yupo
madarakani, lakini tangu Desemba mwaka jana, yeye sio mkuu tena wa ANC.
Waendesha mashtaka
wakakamavu sasa wanaonekana kushika kasi katika uchunguzi dhidi ya tuhuma za
rushwa zinazomkabili bwana Zuma na baadhi ya marafaiki zake wa karibu.
Wengi ndani ya ANC
wanamtaka rais huyo ajiuzulu haraka iwezekanavyo, ili waweze kulenga kujenga
upya sifa ya chama hicho kufuatia kuwadia kwa uchaguzi mkuu nchini mwakani.
Lakini kuna taarifa
kwamba Zuma anajikita kisawasawa.
Anatarajiwa kulihotubia
bunge wiki ijayo, lakini wafuasi wa upinzani wanataka kumzuia pia, wakieleza
kuwa hastahili kusalia kama rais.
Kiongozi mpya wa ANC,
Cyril Ramaphosa, ameshutumu wazi rushwa katika kiwango cha juu ndani ya chama
na serikali, lakini anasisitiza kuwa rais Zuma hastahili kuazirishwa.
No comments:
Post a Comment