Dkt .Lauren Ndumbaro, katibu Mkuu Ofisi ya Rais , Manajimenti ya Utmishi wa Umma |
Serikali imewasimamisha kazi maofisa utumishi watano wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza kwa kosa la kutosimamia vema uhakiki wa vyeti vya ufaulu wa elimu ya kidato cha nne, sita na ualimu.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala wa Bora, DkLaurean Ndumbaro ametoa maelekezo kwa Mkurugenzi Mtendaji
wa Halmashuri ya Wilaya ya Kwimba, Pendo Malabeja kuwasimamisha kazi na
kuwachukulia hatua za kinidhamu maofisa utumishi hao.
Serikali imewasimamisha kazi maofisa utumishi watano wa
Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza kwa kosa la kutosimamia vema
uhakiki wa vyeti vya ufaulu wa elimu ya kidato cha nne, sita na ualimu.
Kwa mujibu wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Dk Ndumbaro ametoa maelekezo hayo, baada ya kufanya ziara ya
kikazi katika Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba. Maofisa waliosimamishwa kazi ni
Mkuu wa Idara ya Utawala na Rasilimaliwatu, Christina Bunini na wasaidizi wake
wanne ambao ni Edward Cornel, Rey Lema, Julius Kiduli na Clavery R.M.
Dk Ndumbaro alisema maofisa hao wameitia serikali hasara kwa
kuwaacha watumishi wasio na sifa kuendelea kuwepo kwenye orodha ya mishahara ya
watumishi wa serikali. Taarifa hiyo ya Utumishi iliwataja miongoni mwa
watumishi walioachwa ni Ligwa Simon aliyestaafu kwa hiari Januari 4, 2010 na
Fundi Sanifu Mkuu, Kalala Seleman ambaye amekiri kufanya udanganyifu kwa Katibu
Mkuu, Dk Ndumbaro baada ya kukutana naye katika Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa
Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba.
Katibu Mkuu alijiridhisha kuwa maofisa utumishi hao kutozingatia
maelekezo ya kuwaondoa watumishi ambao taarifa zao walizojaza wakati
wanaajiriwa zinaonesha kuwa wamehitimu na kufaulu kidato cha nne, lakini wakati
wa uhakiki, watumishi hao hawakutakiwa kuwasilisha vyeti husika kwa kigezo kuwa
wana elimu ya darasa la saba.
Taarifa hiyo ilieleza kuwa kwa msingi huo na kwa kuzingatia kuwa
maofisa utumishi hawakuwataka watumishi hao kuwasilisha vyeti vya elimu
walizojaza wakati wanaajiriwa katika fomu ya taarifa binafsi, wamekiuka na
kupuuza agizo la Rais John Magufuli la kuwataka waajiri wote nchini kufanya
uhakiki wa vyeti vya watumishi wa umma na kuwaondoa katika orodha ya malipo ya
mshahara ya watumishi wa serikali (Payroll).
Dk Ndumbaro alimtaka Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza, Kamishna wa
Polisi, Clodwing Mtweve kupeleka maofisa utumishi wengine katika Halmashauri ya
Kwimba ili kutoathiri utendaji kazi. Pia aliwataka waajiri wote nchini
kuhakikisha kazi ya uhakiki wa vyeti vya watumishi inafanyika kwa umakini.
Aidha, Dk Ndumbaro aliainisha kuwa, suala hilo litawasilishwa kwa mamlaka ya
uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba, Pendo
Malabeja kuona hatua stahiki za kuchukuliwa dhidi yake.
No comments:
Post a Comment