Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt Rehema Nchimbi |
Mkuu
wa Mkoa wa Singida, Dk Rehema Nchimbi
ametoa miezi minne kuanzia sasa kwa uongozi wa vijiji na kata kuhakikisha
wanatunga sheria ndogo ya kunyonyesha ili kuondokana na tatizo la ukosefu wa
lishe kwa watoto mkoani humno.
Dk Nchimbi alitoa agizo
hilo juzi wakati wa hafla ya kukabidhiwa vifaa vya kutambua hali ya lishe kwa
watoto na akinamama wajawazito katika kijiji cha Saranda wilayani Manyoni.
Alilazimika kutoa agizo
hilo baada ya kusomewa taarifa inayoonesha kuwa ni asilimia 54 tu ya watoto
mkoani Singida ndio hubahatika kunyonyeshwa maziwa ya mama pekee kwa kipindi
cha miezi sita.
Alisema kuwa suala la
kunyonyesha siyo la hiari kwa kuwa kutokufanya hivyo kunahatarisha afya ya
mtoto. “Kunyonyesha ni lazima. Wenyeviti wa vijiji na kata hakikisheni mmetunga
sheria ndogo kwa ajili ya kudhibiti akinamama wote wasionyonyesha watoto wao
kulingana na taratibu za afya.”
Nchimbi alisema kuwa
ulazima huo usibakie kuwa ni wa majukwaani tu bali utekelezwe kisheria na
atakayepatikana aadhibiwe, hata hivyo, mhakikishe adhabu hiyo haisababishi mama
kumkimbia mtoto.
Aidha, Dk Nchimbi
aliagiza pia itungwe Sheria ndogo kwa ajili ya kuwapatia wanafunzi chakula cha
mchana wawapo shuleni. Aliwataka pia viongozi wa dini kuhubiri suala la lishe
akidai kuwa mahubiri hayawezi kumwingia vyema muumini asiye na lishe njema.
No comments:
Post a Comment