Shirika
la afya duniani WHO linasema saratani ndio chanzo cha kifo cha mtu mmoja kati
ya sita duniani, na hadi 50% ya aina zote za saratani zinaweza kuzuilika.
Lakini
idadi ya visa vipya vya ugonjwa huo inatarajiwa kuongezeka kwa takriban
asilimia sabiini katika miongo miwili ijayo.
Utumiaji tumbaku ndio
hatari kuu ya chanzo cha kuugua saratani na ndio chanzo cha takriban 22% ya
vifo jumla vinavyotokana na saratani.
Saratani ya matiti
inaongezeka, hususan katika mataifa yanayoendelea, ambapo visa vingi hutambuliwa
katika awamu ya mwisho wakati ugonjwa tayari umesambaa mwilini mwa muathiriwa.
Mambo kumi unayoweza
kufanya kupunguza hatari ya kuugua saratani:
§
Usivute sigara wala
kutumia tumbaku ya aina yoyote
§
Hakikisha nyumbani
kwako hamna moshi
§
Kula chakula chenye
afya
§
Kunyonyesha
kunapunguza hatari kwa mama kuugua saratani
§
Hakikisha watoto wako
wanapata chanjo dhidi ya hepatatis B na HPV
§
Epuka kuchomwa sana na
miale ya jua, au tumia mafuta yanayo kukinga dhidi ya miale hiyo.
§
Punguza uchafuzi wa
hewa ndani na nje ya nyumba
§
Jishughulishe kuupa
mwili mazoezi
§
Punguza unywaji wa
pombe
§
Jitahidi kufanyiwa
ukaguzi wa mapema kutambua uwepo wa saratani.
huko nchini Kenya, ni ugonjwa
wa pili unaochangia vifo vya watu baada ya magonjwa ya moyo
- Licha ya kuidhinishwa
kwa baadhi ya malipo ya matibabu katika bima ya kitaifa ya afya nchini, bado
tatizo lipo kutokana na kutowepo kwa taasisi za kutosha za umma zinazotoa
huduma hizo - na kwa chache zilizopo, hazina vifaa vya kisawasawa.
-Ni wachache wanaoweza
kumudu gharama kubwa katika hospitali za kibinafsi.
- Tanzania hali sio
tofauti sana, wakati kunashuhudiwa uhaba wa vituo vya kutibu wagonjwa wa
saratani - kuhudumia idadi jumla ya zaidi ya watu milioni 50 nchini .
- Takwimu zinaonyesha kuwa
saratani ya mfuko wa uzazi ni chanzo kikuu kwa wanawake wanaougua saratani
Tanzania.
- Kwa mujibu wa taasisi ya
habari kuhusu kirusi cha HPV na saratani #ICO - tofauti na saratani nyingine,
saratani ya mfuko wa uzazi inaweza kutambuliwa na kuzuiwa kabla ishike kasi na
kusamabaa kwa ukubwa.
No comments:
Post a Comment