SHAMBULIO LA FLORIDA, TRUMP ALAUMIWA - NIJUZE NEWS

Breaking news

Nyumba ya Habari Makini na za Uhakika

Pata Habari Mpya kwa kina Kila muda kutoka kwanye vyanzo vya Uhakika

Mikoani leo

Mikoani leo

Friday, February 16, 2018

SHAMBULIO LA FLORIDA, TRUMP ALAUMIWA

Chama cha Democrats kimewashutumu Rais Donald Trump na Spika wa bunge la nchi hiyo Paul Ryan kwa kukataa kuruhusu mjadala wa sheria ya kumiliki silaha.
Hii imetokea siku moja baada ya wanafunzi 17 kuuawa kwa kupigwa risasi huko Marekani.
Wakati huo huo shughuli ya kuwasha mishumaa kuwakumbuka waliouawa kwenye tukio hilo imefanyika huko Florida kulikotokea tukio hilo.
Image result for picha za trump
Donald Trump, Rais wa Marekani


Wakati wa Marekani wakiwa bado wanaendelea kuomboleza kifo cha wanafunzi 17 waliuawa kwa kupigwa risasi kumekuwa na wito wa nchi hiyo kubadili sheria ya kumiliki silaha.
Akizungumzia mauaji hayo Rais wa Marekani Donald Trump awali katika hotuba yake amesema usalama katika shule utakuwa ni moja ya mambo yatakayopewa kipau mbele.
Hata hivyo alishindwa kulishauri bunge la nchi hiyo lipitie upya sheria ya kumiliki silaha.
"Utawala wetu unafanya kazi kwa karibu na mamlaka za eneo la mji kuchunguza tukio la kupigwa risasi na kupata taarifa zote iwezekanavyo. Tumejitolea kufanya kazi na jimbo pamoja na viongozi wa eneo hilo kusaidia kulinda usalama wa shule na kukabiliana na masuala magumu yanayotokana na matatizo ya afya ya akili." alisema Rais Trump
Shughuli ya kuwasha mishumaa kuwakumbuka waliouwawa
Waombolezaji wa Shambulio, ka Florida

Siku ya Jumatano watu 17 waliuawa kwa kupigwa risasi na mwanafunzi aliyefukuzwa shule kwa utovu wa nidhamu katika shule moja huko katika jimbo la Florida.\
Akihutubia katika tukio hilo Baba wa mwanafunzi wa miaka 14 aliyeuawa kwenye tukio hilo Fred Guttenberg amesema familia yake imeumia kutoka na kifo mtoto wao.
Mtuhumiwa huyo akifika mbele ya mahakama kusikiliza mashtaka
Mtuhumiwa wa Shambulio la Florida
"Haina maana. Hii haiwezekani. binti yangu , mtoto wangu mwenye umri wa miaka 14. na kwenu mnaojua binti yangu Jamie, alikuwa ni maisha katika burudani. Alikuwa anatutia nguvu tukio nyumbani.

No comments:

Post a Comment

Mikoani leo

Mikoani leo