Hassan Abuutwalib Mitumishi wa TRA(Picha ya Mtandao) |
Mtumishi wa Mamlaka ya
Mapato Tanzania (TRA), Hassan Abuutwalib maarufu Kiringo anashikiliwa na Jeshi
la Polisi Zanzibar kwa tuhuma za kumlawiti mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka
13.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, Hassan
Nassir Ali amesema wamemkamata Februari 18, 2018 katika maeneo ya Uwanja wa
Ndege Zanzibar alipokuwa akijaribu kuondokea Mwanza.
Kamanda Nassir amesema Kiringo anatuhumiwa kumlawiti mtoto wa
miaka 13 baada ya baba wa mtoto huyo jina limehifadhiwa mwenye miaka 54
kuripoti polisi kuwa mtoto wake alichukuliwa na Kiringo na kumpeleka katika
nyumba iliyokuwa haijamalizwa kujengwa huko Fuoni Uwandani ambapo alimlawiti
baada ya kumpa dawa za kupoteza fahamu na kumsababishia maumivu makali ambapo
ripoti ya uchunguzi wa madaktari ilithibitisha kuathirika sehemu za siri za
nyuma za mtoto huyo.
Aidha, Kamanda Nasiri amesema ameunda timu ya uchunguzi
iliyojumuisha wakuu wa upelelezi wa wilaya tatu Wilaya ya Mjini, Wilaya ya
Magharibi A na B kufanya uchunguzi juu ya suala hilo zito ambalo ameshindwa
kulifumbia macho.
Kiringo aliwahi kushutumiwa kwa matukio tofauti ya kulawiti
kabla ya tukio hili, wananchi wamekuwa wakipiga kelele kwa kuwaharibia vijana
wao.
Februari Mwaka 2012, wazanzibari waliwahi kumlalamikia kwa
Vyombo vya Dola kwa vitendo vyake hivi:
Hassan Aboud Talib umaarufu Hassan Kiringo, kijana ni mmoja
katika vijana wenye akili ya kuzaliwa, baba yake alikuwa ni waziri kiongozi
katika awamu ya pili wakati wa uongozi Aboud Jumbe. Huyu ni kijana aliyekulia
Michenzani jumba nambari tano, alisoma shule ya Vikokotoni, kwa wakati ule ndie
aliyekuwa mwanafunzi aliyepasi vizuri kwa Unguja na Pemba katika kidato cha
tatu ndiye alikuwa mwanafunzi bora, na kuendelea na masomo yake shule ya
Lumumba na kupata divison 1. Alisoma PCM form six na hatimaye kufutiwa matokeo
yake.
Tunayaandika haya na kumtaja Kiringo kwa kutoa mfano wa jamii
yetu ilivyoharibika. Huyu ni mfanyakazi wa Idara ya Mapato kwa hiyo shughuli ya
pesa kwake sio kubwa kwani kuchota fedha ya serikali sio tatizo kubwa kwake.
Ilifikia wakati alikuwa akiwanunulia vijana hadi vespa na kuwanunulia na
kumwaga fedha za kiwango cha juu ili apate analolitaka kuwalawiti vijana hao.
Je, kweli nani asiyemjua Kiringo kuwa alikuwa anakaa kinyumba
na mtoto wa kiume kama mkewe pale jumba nambari nne Michenzani? Je, kweli
hakuna anayeliona hili? Na je hujawahi watu kumuona wanachanganyikana nae
maskani au sehemu nyingine?
Hivyo, kweli mtu kama huyu na wenzake wengine ambao wao
wamekataa kata kata umbile bora la kike aliloumba Allah na kuchukuwa wanaume na
kufata kaumu ya Luti? Lakini kwa vile sisi tumeona ni maendeleo basi tunakaa
pembeni na kuyatizama haya. Je, jiulize kweli kwa hali hii umasikini, ufukara na
shida zitaondoka visiwani?
Na huyu ni mmoja tu kati ya wengi, kuna Ahmada ambae mkaazi
wa Majestic Vuga nyuma pale ya Cinema yeye ndie aliemharibu marehemu Omar Kopa
mpaka wakati wa kifo chake, je hili lilikuwa halionekani? Na ilikuwa ukipita
Majestic watu wanakaa nae na kufurahi nae na baada ya hapo unaelekea msikitini
kusali, je nani unamdanganya?Unamdanganya Allah au unaidanganya nafsi yako.
No comments:
Post a Comment