Kufuatia
kauli iliyotolewa na Askofu Zachary Kakobe wa Kaninisa la Full Gospel Bible
Fellowship katika mahubiri ya lbada ambayo alisema kuwa "Yeye ana pesa kuliko Serikali
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania", Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ilifanya uchunguzi
ili kubaini usahihi wa kauli hiyo.
Yafuatayo ni mambo ambayo yalibainika baada ya kufanyika
uchunguzi kuhusu kauli ya Askofu Zachary Kakobe,
1. Askofu Zachary Kakobe hana akaunti wala fedha katika Taasisi
yoyote ya fedha hapa nchini. Aidha uchunguzi ulibaini kuwa Askofu Kakobe ni
mmoja wa wasimamizi wakuu wa akaunti za kanisa (signatories) zilizopo katika
benki ya NBC zenye jumla ya kiasi cha shilingi 8,132,100,819.00, kiasi hicho
cha fedha kimetokana na sadaka, zaka na changizo ambazo zinatolewa na waumini
wa kanisa tajwa hapo juu, hivyo kwa mujibu wa Sheria hakitozwi kodi.
2. Kanisa Iilikwepa kulipa kodi kiasi cha shilingi
20,834,843.00 ambazo zilitokana na uwekezaji katika makampuni ya kukuza mitaji.
Kodi hiyo imelipwa baada ya uchunguzi.
3. Kampuni inayomilikiwa na watoto wa Askofu Zachary Kakobe
ilikwepa kulipa kodi Idasi tha shilingi 37,280,030.00 ambazo zimelipwa baada ya
uthunguzi. Kwa ujumla, kiasi cha kodi kilicholipwa kutokana na uchunguzi huu ni
shilingi 58,114,873.00.
4. Kanisa linatunza kiasi kikubwa cha fedha kwenye ndoo na
'majaba' kinyume na taratibu za utunzaji wa fedha, lakini pia uwekaji na utoaji
wa fedha nyingi kutoka benki haushirikishi vyombo vya ulinzi na usalama kwa
ajili ya usalama wa fedha zenyewe na wahusika.
5. Pia ilibainika kwamba Kanisa halitengenezi hesabu za
Mapato na Matumizi ya Fedha kitu ambacho ni kinyume na Katiba ya Kanisa pamoja
na sheria za usimamizi wafedha arnbayo imepelekea matumizi mabaya ya fedha za
waumini kama vile safari za nje ya nchi ambazo zimedhaminiwa na kanisa lakini
wanaosafiri ni Askofu na familia yake. Vile vile fedha za Kanisa zinatumika
kujenga nyumba ya mke wa Askofu, kwa jina lake na wala si kwa jina la Kanisa,
kitu ambacho ni kinyume na taratibu za Kanisa.
Aidha, wakati uchunguzi huo ukiendelea, mnamo tarehe
24.01.2018 Askofu Kakobe aliandika barua kwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kuomba radhi kutokana na Kauli yake ya kebehi pamoja na
matamshi yake ya dharau kwamba ana pesa nyingi kuliko Serikali
WITO:
• Mamlaka ya Mapato Tanzania inatoa wito kwa Taasisi zote za
dini ambazo zinajihusisha na shughuli zozote za kiuchumi kulipa kodi stahiki na
kwa wakati kwa mujibu wa sheria, kanununi na taratibu za kodi.
• Mamlaka ya Mapato Tanzania inazitaka Taasisi zote za kidini
kufuata katiba zao ikiwa ni pamoja na kutengeneza hesabu za mapato na matumizi.
Charles E. Kichere
KAMISHNA MKUU MAMLA. YA MAPATO TANZANIA
"Pamoja Tunajenga Taifa Letu"
No comments:
Post a Comment