Ndugu wa Mareheu wakikusanyika |
Wakinukuliwa na Shirika la Utangazaji la BBC, ndugu wa marehemu Damian Swai, amesema
wanasubiri matokeo ya uchunguzi wa polisi ili waone hatua ambayo itafaa
kuchukuliwa.
Damian ameendelea kusema kuwa marehemu alikuwa na ndoto za
kusoma na kufaulu na kuwa na maisha yake vizuri lakini, "ndoto yake
imekatishwa."
Waombolezaji wakikusanyika nyumbani kwa marehem Akwilina Mbezi Luis Jijini Dar es Salaam |
Taarifa za kifo cha mwanafunzi huyo zilifikia familia kupita
Chuo cha Usafirishaji cha NIT ambapo alikuwa anasoma.
Mwili wa marehemu unategemewa kusafirishwa hadi Rombo, Moshi,
Mkoani Kilimanjaro kwa wazazi wake ambapo ndipo atakapozikwa.
Hata hivyo, serikali kupitia Waziri wa Elimu imesema itagharamia
mazishi ya mwanafunzi huyo.
Nae
dadake marehemu ameomba "haki itendeke" ili waliohusika na kifo chake
wachukuliwe hatua za kisheria.
Hadi sasa polisi 6 wamekamatwa kuhusiana na kifo cha mwanafunzi
huyo.
Kumekuwa na shinikizo kutoka vyama vya upinzani kama vile
chama cha ACT Wazalendo, vijana na Shirika la wanafunzi nchini limemtaka waziri
wa maswala ndani nchini humo Mwigulu Nchemba kuchukua jukumu la kisiasa na
kujiuzulu kufuatia kisa hicho.
No comments:
Post a Comment