Madini ya dhahabu (Getty Image/mtandao) |
Mwanamume
huyo mwenye umri wa miaka 46 anadaiwa kuwasili kutoka Mwanza, Tanzania kupitia
uwanja wa Kilimanjaro na alikuwa safarini kuelekea Dubai.
Gazeti la kibinafsi
ya Nation linasema mwanamume huyo, ambaye jina lake halijafichuliwa kufikia
sasa, aliwasili uwanja wa JKIA Ijumaa 16 Februari ndege ya abiri ya Precision Airlines na alitaka kupanda ndege
ya abiria ya Kenya Airways kuelekea Dubai.
Maafisa
wa uIdara ya Uchunguzi wa Jinai wakiandamana na maafisa wa uchunguzi kutoka
Mamlaka ya Mapato ya Kenya (KRA) walimhoji na akaandikisha taarifa.
Mtanzania huyo
amekamatwa kwa sababu Sheria za Usimamizi wa Forodha za Jumuiya ya Afrika
Mashariki (EAC) za mwaka 2004, kKifungu 85(3) na Kiambatisho cha Pili Sehemu B
(4) huharamisha usafirishaji wa madini ambayo hayajapitia viwandani katika
kanda ya Afrika Mashariki.
Vipande hivyo vya
dhahabu vya uzani wa kilo 32.3 vinashikiliwa na maafisa wa idara ya forodha wa
KRA huku uchunguzi zaidi ukiendelea.
No comments:
Post a Comment