Wafuasi wa Raila Odinga wakisubiri kuapishwa kwake |
Mgombea
mwenza wake Kalonzo Musyoka wa chama cha Wiper hakujitokeza katiaka sherehe hiyo ya kuapishwa, ingawa alikuwa
miongoni mwa waliotarajiwa kuapishwa kuku Raila akisema kuwa, ataapishwa
"baadaye".
Ifuatayo ni Orodha wa Watu Waliowahi kujiapisha Wenyewe
Ettiene Tshekedi -DRC (Picha ya Mtandao) |
Etienne Tshisekedi
alikuwa kiongozi mkuu wa upinzani, wakati wa utawala wa Rais Mobutu Sese Seko
Zaire, na baadaye Laurent Kabila Joseph Kabila wa DRC
Kufanana
kati ya Tshisekedi na Odinga ni kwamba wote wawili walikuwa kizuizini bila
kufunguliwa mashtaka, wote walihudumu kama mawaziri wakuu na wote waligomea
uchaguzi wa urais; Tshisekedi mwaka 2006, Odinga katika 2017.
Mwezi
Novemba 2011, Tshisekedi alijitosa kwenye kinyang'anyiro dhidi ya mtoto wa
Laurent Kabila, kisha aliamua kujiandalia kiapo mwenyewe na kuapishwa nyumbani
kwake na mkuu wa watumishi wake Albert Moleka baada ya jaribio la kujiapisha
katika uwanja wa Wahanga, Kinshasa kutibuka. Baadaye, aliwekwa katika kizuizi
cha nyumbani.
Moshood Abiola- Nigeria (Picha ya Mtandao/AFP) |
Nigeria, Moshood Abiola
alijitangaza mwenyewe kuwa rais kipindi ambacho Rais Sani Abacha alipokuwa
madarakani.
Hii
ni baada ya kutembelea nchi nyingi za Magharibi, kutafuta msaada ili kumkabili
Abacha katika utawala wake.
Alikamatwa
na kushtakiwa kwa uhaini na kufungwa jela kwa miaka minne hadi ilipofika mwaka
1995, Siku aliyoachiwa kutoka gerezani, alikutana na ujumbe wa Marekani na
kuhuduria mkutano.
Baada
ya kupewa chai akiwa mkutanoni alianguka na kuzimia na hatimaye kufariki dunia.
Jean Ping -Gabon (Picha ya Mtandao/AFP |
Mwaka 2016 Gabon,
kiongozi wa upinzani Jean Ping alijitangaza mwenyewe kuwa rais na kutoa wito
kura kurudiwa kuhesabiwa kwa kura ambazo zilithibitisha kwamba Ali Bongo
ameshinda. Hata
hivyo dunia nzima alijua kwamba Ping ndiye alikuwa rais wa nchi hiyo
Dkt Kiiza Besigye- Ugada (Getty Image) |
Nchini
Uganda Kiongozi wa upinzani Kizza Besigye, ambaye ni mpinzani wa muda mrefu wa
Rais Yoweri Museveni, kupitia kanda ya video alionekana akifanya sherehe za
kula kiapo kuwa Rais wa Uganda baada yake kushindwa uchaguzini mwaka 2016 na Bw
Museveni.
Alikamatwa
na kufunguliwa mashtaka ya uhaini.
Bw
Besigye amekuwa akikamatwa na kushtakiwa mara kwa mara nchini humo.
.
No comments:
Post a Comment