Mazavi yasiyo na heshimi mbele ya jamii yanaendelea kupinwa kila mahali baada ya Jumuiyaya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Meru mkoani Arusha, imesema
ni marufuku wanafunzi wa shule za Msingi na Sekondari kwa wasichana kuvaa sketi
fupi na wavulana kunyoa viduku, kuvaa suruali chini ya makalio ili kulinda na
kutunza maadili ya Kitanzania.
Pia jumuiya
hiyo imempongeza Rais John Magufuli kwa kupiga marufuku wazazi kuchangishwa
michango mbalimbali kwa shule za serikali za msingi na sekondari nchini.
Pongezi hizo zimetolewa jana na Mwenyekiti wa jumuiya hiyo wilayani Meru, Simon
Kaaya jana wakati wa ziara yake ya kikazi alipotembelea shule za msingi na
sekondari, kwenye Kata ya Ambureni.
Alisema
baadhi ya shule walimu walikuwa siyo waadilifu ambapo walikuwa wanachangisha
michango hiyo wakati mwingine hata kwa ajili ya chai za walimu. Kwa mujibu wa
Kaaya, kuondolewa kwa michango hiyo kumesaidia wazazi kupata faraja kubwa na
kuishukuru serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Dk Magufuli anayehangaika
na shida za wananchi wanyonge.
Kuhusu sare
za shule za wanafunzi wilayani humo kutokidhi maadili ya kitanzania, Mwenyekiti
huyo aliwataka wasimamie kikamilifu kuhakikisha hakuna wanafunzi wa kike
wanaovaa sketi fupi za mlegezo au wavulana wanaovaa suruali mlegezo zilizobana
miguuni pamoja na kunyoa kiduku. “Sisi kama wazazi jukumu letu kubwa ni
kuhakikisha maadili mema yanazingatiwa haswa na watoto wetu kwa ajili ya
kutunza heshima ya nchi yetu.
Tutaisimamia
serikali wilayani hapa kuhakikisha inachukua hatua kali za kisheria dhidi ya
wanafunzi wote wanaovaa nguo ambazo hazina heshima.” Alisema jumuiya ya wazazi
moja ya jukumu lake kubwa ni kutoa malezi bora kwa jamii nzima ikiwemo watoto
na vijana na kwamba ni jukumu lao kuhakikisha watoto na viajana wanakuwa na
maadili mema katika jamii inayowazunguka.
No comments:
Post a Comment