Wakazi wa Mkoa wa Katavi wamepigwa na Mshangao baada ya
Mwanafunzi wa kike mwenye umri wa miaka 14 ameuawa kikatili baada ya kubakwa
kwa zamu na mwendesha pikipiki maarufu ‘bodaboda’ kisha akachomwa kisu ubavuni
na sehemu zake za siri kunyofolewa wakati akienda shule akiwa amefuatana na
mdogo wake wa kiume mwenye umri wa miaka 11.
Mwanafunzi huyo alikuwa akisoma darasa la sita katika Shule ya
Msingi Vikonge katika wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi, sambamba na mdogo
wake wa kiume ambaye alikuwa akisoma darasa la nne kwenye shule hiyo. Kamanda
wa Polisi mkoa wa Katavi, Damas Nyanda alisema kuwa tukio hilo la kikatili
lilitokea juzi Jumanne saa moja asubuhi umbali wa kilometa moja na nusu kutoka
shuleni hapo.
“Asubuhi hiyo ya tukio, marehemu akiwa ameongozana na mdogo wake
wa kiume huku wakielekea shuleni walikutana na mwendesha pikipiki maarufu
‘bodaboda’ ambaye alikuwa hawamfahamu na kuwaambia kwamba atawapa lifti.
Marehemu alipopanda
mwendesha bodaboda alimzuia mdogo wake wa kiume asipande ambapo aliondoka
akiendesha pikipiki hiyo kwa kasi isiyo ya kawaida huku kaka wa marehemu
akiikimbilia bila mafaniko.
Aliongeza kuwa mdogo wa marehemu alipoamua kutembea kwa miguu
kuelekea shuleni baada ya kuchoka kuifukuza pikipiki hiyo, ghafla aliiona
pikipiki ile iliyombeba dada yake ikiwa imeegeshwa karibu na kichaka kando ya
barabara inayoelekea shuleni kwao na akaipita.
Kamanda Nyanda alisema kaka huyo wa marehemu alienda shuleni
hapo na kuhudhuria darasani kama kawaida hadi ilipofika saa nane na nusu
alianza safari kuelekea nyumba pasipo kumtafuta dada yake.
“Kaka wa marehemu bila shaka kutokana na umri wake kuwa bado
mdogo baada ya kufika shuleni hakushughulika kumtafuta dada yake, aliingia
darasani na kuendelea na masomo kama kawaida na baada ya muda wa masomo yaani
saa nane na nusu alianza safari ya kurejea nyumbani bila kumtafuta dada yake,”
alieleza Kamanda Nyanda.
Aliongeza kuwa baada ya mtoto huyo kufika nyumbani wazazi wake
walishtuka kumuona akiwa pekee yake ndipo walipomuhoji alikomuacha dada yake
ndipo alipowasimulia kila kitu.
“Wazazi wa marehemu baada ya kupata maelezo hayo walipatwa na
mashaka hivyo walimtaka mdogo wa marehemu awapeleke kwenye eneo alipoina
pikipiki iliyombeba dada yake ikiwa imepakiwa karibu na kichaka.
Mtoto huyo aliwaongoza wazazi wake ambao walikuwa wamefutana na
majirani zao hadi kwenye eneo la tukio, walishtuka kuona kuwa kuna nyasi
zilikuwa zimelala ndipo walipoona mwili wa marehemu ukiwa umechomwa kisu
ubavuni huku sehemu zake za siri zikiwa zimenyofolewa.
No comments:
Post a Comment