![]() |
| Refa Tony Chapron alienyoosha mguu |
PSG, Ufaransa
Mechi kati ya Paris St-Germain na klabu ya Nantes nchini Ufaransa ilikumbwa na utata baada ya mwamuzi kuonekana kumrushia teke mchezaji.
Mwamuzi huyo Tony Chapron alifanya hivyo baada yake kugongana na mchezaji huyo Diego Carlos.
Baada ya hilo, alimlisha mchezaji hiyo kadi ya pili ya manjano na kumfukuza uwanjani kufuatia kisa hicho muda wa ziada wa mechi.
Mwenyekiti wa Nantes Waldemar Kita amesema Chapron anafaa kupigwa marufuku kwa miezi sita kwa sababu ya uamuzi huo wenye utata.
Ameongeza kuwa: "Sitaki kuamini kwamba alifanya hivyo makusudi."
PSG walipokuwa wanashambulia eneo la hatari la Nantes, Carlos alimgonga Chapron kwenye kisigino katika kile kinachoonekana kuwa ajali.
"Ni mzaha," Kita aliambia runinga moja ya Ufaransa.
"Nimepokea arafa 20 kutoka pande mbalimbali duniani kuniambia kwamba huyu mwamuzi ni mzaha tu.
"Nikizungumzia hili sana, nitaitwa kujibu maswali na kamati ya maadili. Hatuna haki ya kusema chochote."
PSG walishinda mechi hiyo yao ya kwanza baada ya mapumziko ya msimu wa baridi, bao lao pekee likifungwa na Angel di Maria dakika ya 12 uwanjani Stade de la Beaujoire.
Ushindi huo, bila mchezaji wao ghali zaidi Neymar aliyenunuliwa £200m - uliwaweka alama 11 mbele kileleni Ligue 1

No comments:
Post a Comment