Mjue Milionea msomi Aliyeacha Kuajiriwa na Kuanza Kilimo - NIJUZE NEWS

Breaking news

Nyumba ya Habari Makini na za Uhakika

Pata Habari Mpya kwa kina Kila muda kutoka kwanye vyanzo vya Uhakika

Mikoani leo

Mikoani leo

Thursday, January 18, 2018

Mjue Milionea msomi Aliyeacha Kuajiriwa na Kuanza Kilimo

Annie Nyaga amefanya kitu
ambacho kimebadiisha fikra za
watu wengi hasa vijana wa
kiafrika,na hii ilikuja baada ya
jina lake kuchomoza katika
orodha ya vijana mamilionea
nchini Kenya wakati huo akiwa
hajulikani na mtu yeyote
kabisa.Akiwa na digrii yake ya
kwanza ya Biomedical Science
and Technology kutoka chuo
kikuu cha Egerton aljikuta
amekataa scholarship aliyopewa
ya kwenda kusoma Marekani ili
aiishi ndoto yake ya kuwa
mkulima.Annie wakati ameibuka
kuwa milionea alikuwa ni binti
kijana wa miaka 29 lakini
maisha yake yamebadilika sana
kwa kuamua kuishi kitu
ambacho moyo wake ulikuwa
unakitamani kila siku.
Annie kwa sasa haishi
mjini,anaishi kijijini kwake kwa
asili Mbeere,Embu Kaunti
ambako analima matikiti
maji,nyanya pamoja na mazao
mengine.Kwa sasa shamba lake
limekuwa la kisasa likiwa na
mashine mbalimbali na
wafanyakazi kadhaa walio chini
yake,yeye akiwa ni mkurugenzi
wa kampuni yake aliyoianzisha
ya Farm2Home.Kabla ya
kuamua kuwa mkulima Annie
alikuwa ni afisa ugavi na
baadaye alikuwa anatembeza
bidhaa kuuza kwenye maduka
mbalimbali jijini Nairobi kama
ambavyo vijana wengi
wanafanya katika miji mikubwa.
Habari ya Anne inafanana na
maisha ya watu wengi sana na
kuna mambo kadhaa ya
kujifunza kutoka katika maisha
yake.
Moja ni kuwa,pamoja na usomi
wake Annie aliamua kuiishi
ndoto yake;yaani lile jambo
ambalo alikuwa analiota
kulifanya tangu akiwa na umri
mdogo.Hakuruhusu masomo
aliyosoma chuo kikuu yawe ni
kikwazo kwa yeye kuifuata ndoto
yake.Elimu kazi yake ni kutupa
maarifa ya ziada ili tufanye kwa
ubora mambo tuliyoamua
kuyaishi.Kuna watu wengi leo
ndani ya moyo wao kuna kitu
wanatamani kufanya lakini
wameendelea kung’ang’ania
kukabwa na taaluma zao eti kwa
sababu tu walisomea.Ni lazima
ujue kuwa watu wanaofanikiwa
haraka ni wale ambao
wanafanya kitu ambacho
kinagusa moyo wao,wanaishi
katika “Passion yao”.Usione
haya kufanya kazi inayoonekana
sio ya kisomi lakini ina utajiri
ndani yake.
Annie anatufundisha kuwa
tusifuate mkumbo wa maisha.Ni
kawaida kwa vijana wengi
kung’ang’ania mijini mara
baada ya kumaliza masomo yao
vya vyuo.Unakuta miezi kwa
miezi,wengine hadi
miaka,wengine wanathubutu
kukataa nafasi za kazi eti kwa
sababu ziko mikoa mingine
toafuti na Dar es Salaam ama
sio kwenye miji mikubwa.Kuna
fursa nyingi kila mahali,usiwe
mtumwa wa fikra kuwa ili
ufanikiwe lazima urundikane
kwenye miji na wenzako.Angalia
ndoto yako,usijali wengine
watasema nini,chukua hatua
mara moja na anza kuiishi.Annie
aliacha kazi toka kwenye
kampuni ya mauzo na kwenda
kuanza kuishi ndoto yake
kijijini.Na leo amefanikiwa kuliko
wengi aliowaacha mijini.Suala
sio unaishi wapi,suala la
muhimu ni kama uanfanya
jambo ambalo ndio ndoto ya
maisha yako.
Inashangaza kuona kuna watu
wanang’ang’ania kukaa mijini
eti kwa ufahari tu kwamba
wanaishi kwenye majiji lakini
ukichunguza kazi na kipato
wanachopata ukweli ni kuwa
wanasurvive(wanasukuma siku)
wakati kama wangeamua
kuchukua fursa zilizoko nje ya
miji wangefanikiwa.Usiwe mmoja
wao.Kwa sasa Annie ni milionea
anayeishi kijijini.Hivi jambo zuri
ni lipi?Kuishi kitajiri kijijini na
ukawa na uwezo wa kuja mjini
wakati wowote unaotaka tena
kwa ndege ama kuishi mjini
huku ukiugulia maumivu ya
maisha na hata mzazi akiomba
hela ya vocha hauna?Uchaguzi
ni wako.
Jambo lingine analotufundisha
Annie ni ukweli kuwa tunahitaji
kuwa wavumilivu ili kutimiza
ndoto zetu.Katika mahojiano
Annie alieleza kuwa amekutana
na changamoto mbalimbali
ikiwezo ya kubadilika kwa bei ya
mazao yake na pia ukosefu wa
mvua za wakati.Kiufupi ni kuwa
hakuna ndoto ambayo
haitakabiliwa na changamoto
utakapoanza kuitekeleza.Ni
lazima ufanye uamuzi tangia
mwanzo unapoanza kuchukua
hatua kuwa hautakata tamaa.
Ni lazima ujue kuwa kuna watu
watakucheka,wengine
watakudhihaki,wengine
watakushangaa lakini kama ni
ndoto umeiamini ni lazima
uamue kukabiliana na vitu vyote
hivyo katika maisha
yako.Jiulize?je unaishi ndoto
yako leo?ama unaishi maisha ya
kuwafurahisha wengine huku
ndani yako unaumia?FANYA
MAAMUZI.
Mafanikio ya kweli yanaanza
pale unapokuwa na ujasiri wa
kuchukua hatua za kuanza
kuiishi ndoto yako.

No comments:

Post a Comment

Mikoani leo

Mikoani leo