Msanii Diamond Platinumz |
Msanii yota wa muziki wa kizazi kipya, Nassib Abdul ‘Diamond
Platinumz’ wa Tanzania, anakusudia kuwekeza nchini Rwanda kwa kujenga kiwanda
cha karanga nchini humo.
Kijana huyo
pia anatafuta nyumba ya kuishi jiji Kigali kwa kuwa jiji hilo ni salama, safi
na anamkubali sana Rais Paul Kagame. Kwa mujibu wa msanii huyo, atakapofungua
kiwanda kitatoa fursa za ajira na kwamba lengo la biashara yake ni zaidi ya
soko.
”…nitafurahi
zaidi kama watu watafurahia bidhaa zangu, lakini zaidi wakipata ajira na
kubadili hali ya maisha yao,” alisema wakati akizungumza na waandishi wa habari
jijini Kigali. Msanii huyo alikwenda Kigali Ijumaa asubuhi kwa safari ya
kibiashara na kijamii.
Alisema,
wasanii wanapaswa kufanya muziki si tu kuburudisha, lakini pia uwe chanzo cha
biashara inayoweza kuwanufaisha watu wengi. “Kuna uwezekano kwa vijana wengi
kunufaishwa na biashara zetu (wanamuziki), iwe kwenye kazi za mauzo yetu au
hata kutengeneza ajira kwa ajili yao mara kiwanda kikianza kazi,” alisema
Diamond.
Alisema,
alikwenda jijini humo kusalimia mashabiki wake mtaani na kuwaonesha kuwa sasa
amekua. “Nipo nilivyo kwa sababu ya muziki wangu. Nimefanikiwa sana, naushukuru
muziki.
“Kwa sasa
nina Diamond Karanga, manukato ya Chibu na Wasafi Records. Nataka pia kufungua
Wasafi FM na Wasafi TV nchini Tanzania,” alisema Diamond.
Alisema amepata mafanikio kwa sababu ya kufanya kazi kwa bidii,
watu anaoshirikiana nao, ubunifu na heshima.
Kupitia vyote
hivi nipo tayari pia kusaidia vijana kukuza vipaji vyao viwe vya kiwango cha
juu kuendeleza muziki wa Afrika,” alisema msanii juyo wa miondoko ya Bongo
Flava.
Jumamosi Diamond
alikwenda kwenye maeneo mbalimbali ya katikati ya jiji la Kigali kutafuta
nyumba ya kununua.
Alikwenda
kuona nyumba kwenye maeneo ya Nyarugenge na Kimihurura.“Mashabiki wangu Kigali
kila mara wananiona jukwaani, nimevaa miwani lakini sasa nataka nitembee kwenye
mitaa ya Kigali, niwasalimie kuwaonesha kwamba kwa kweli nimekua,” alisema
wakati akizungumza na waandishi wa habari.
Nyota huyo wa
muziki aliwasili Kigali asubuhi kwa mwaliko wa Taasisi ya Jordan, inayojitolea
kusaidia watoto wenye matatizo ya kuona kwenye eneo la Gatsata wilayani Gasabo.
Taasisi hiyo ilianzishwa na Vanessa Bahati kusaidia wenye matatizo ya kuona.
No comments:
Post a Comment