URUSI YATISHIA KUJIBU SHAMBULIO LA MAREKANI - NIJUZE NEWS

Breaking news

Nyumba ya Habari Makini na za Uhakika

Pata Habari Mpya kwa kina Kila muda kutoka kwanye vyanzo vya Uhakika

Mikoani leo

Mikoani leo

Friday, April 13, 2018

URUSI YATISHIA KUJIBU SHAMBULIO LA MAREKANI

Image result for picha za Vladimir Putin
Rais wa Urusi- Bw. Vladimir Putin (Picha ya Mtandao)
Urusi imeionya Marekani na washirika wake kuwa hawatasita kuchukua hatua  kama Syria Itashambuliwa kijishi.
Balozi wa Urusi katika Umoja wa Mataifa, Vassily Nebenzia, ameonya kuwa shambulio lolote la anga litakalosababishwa na Marekani nchini Syria litasabaisha kulipuka kwa vita baina ya Moscow na Washington na kuongeza kuwa "hatuwezi kuepuka uwezekano wowote".
Bwana Nebenzia ameituhumu Marekani na washirika wake kwa kuiweka amani ya mataifa katika hati hati kwa kile alichokiita "sera za ukatili" na kuelezea hali ya sasa ilivyo kuwa ni ya hatari kupita kiasi.
Rais Donald Trump wa Marekani anatarajiwa kuwa na mazungumzo na viongozi wa mataifa ya Ufaransa na Uingereza saa kadhaa zijazo kujadili juu ya kutoa kauli ya pamoja kwa kile wanachoamini utumizi wa sialaha za kemikali uliofanywa na Syria kwenye maeneo ya kitalii yanayoshikiliwa na waasi.Ikulu ya Marekani imearifu kwamba mpaka sasa hakuna kauli ya mwisho iliyokwisha fikiwa juu ya hatua za kijeshi zinazoweza kufikiwa.
Ofisi ya Waziri Mkuu wa Uingereza imesema baraza la mawaziri limekubaliana kwamba matumizi ya silaha za kemikali nchini Syria haipaswi kwenda kinyume lakini hakutoa maelezo ya hatua yoyote inayoweza kuchukuliwa.
Baada ya mkutano wa dharula uliochukua saa mbili mjini London, taarifa isiyorasmi unasema kwamba Theresa May ataendelea kushirikiana kikazi na nchi za Marekani na Ufaransa ili kuratibu mwitikio wa kimataifa.
Wabunge kutoka Chama cha upinzani cha Labour pamoja na Chama cha Usimamizi wa kihafidhina wametaka kura ya turufu ipigwe bungeni kabla ya majeshi ya Uingereza kuchukua dhamana.
Mvutano wa Nchi za Mgharibi na Marekani dhidi Urusi unazidi kuzua taharuki ya kuzuka kwa vita, baada ya Shambulia linalodhani kuwa ni la kemikali Mjini Douma wiki kadhaa huku kila nchi zikitupiana lawama juu ya Shambulio hilo.

No comments:

Post a Comment

Mikoani leo

Mikoani leo