MMILIKI WA FACEBOOK AKIRI KAMPUNI YAKE KUINGLILIWA NA URUSI - NIJUZE NEWS

Breaking news

Nyumba ya Habari Makini na za Uhakika

Pata Habari Mpya kwa kina Kila muda kutoka kwanye vyanzo vya Uhakika

Mikoani leo

Mikoani leo

Wednesday, April 11, 2018

MMILIKI WA FACEBOOK AKIRI KAMPUNI YAKE KUINGLILIWA NA URUSI

Nembo ya FacebookMmiliki wa Facebook  Bw. Mark Zuckerberg amkiri kwa mara ya kwanza kwa  maseneta wa Marekani kuwa kampuni yake imekuwa ikipambana na watumiaji wa Warusi wanaotaka kuutumia vibaya mtandao huo wa kijamii
" Haya ni makabiliano ya kijeshi. Watarekebika ,"alisema 
Bw Zuckerberg alikua akijibu maswali kuhusiana na sakata ya matumizi mabaya ya data za kibinafsi maarufu kama Cambridge Analytica.
utokana na hojaji hiyo hisa za mtandao wa Facebook jana ziliongezeka mpaka kufikia asilimia nne
Mkurugenzi wa Mtandao wa facebook Bw. Mark Zuckerberg( Picha ya Mtandao)
Pia amefichua kuwa Robert Mueller, kutoka baraza maalum linalochunguza madai ya Urusi kuingilia uchaguzi wa Marekani wa Mwaka 2016 aliwahoji wafanyakazi wa Facebook.
Bw. Zuckerberg yeye hakuwa miongoni mwa watu waliohojiwa na ofisi ya Bw Mueller
Lakini aliongeza kuwa : "kazi yetu na baraza maalum ni ya siri na ninataka kuhakikisha kwamba katika kikao cha wazi sifichui chochcote juu ya taarifa za siri.
Mwezi Februari, Ofisi ya Bw Mueller ilishtakiwa na Warusi 13 kwa kudukua taarifa za uchaguzi wa mwaka 2016, pamoja na makampuni matatu ya Urusi.
Bw Zuckerberg amesema kuwa kampuni yake sasa imetengeneza nyenzo za kubaini akaunti gushi.
Awali Mtendaji mkuu wa mtandao huo wa kijamii Facebook unaongoza kuwa na watu wengi zaid  ameomba msamaha kwa kamati ya Seneti ya Marekani kwa kuruhusu makampuni kadhaa kutumia vibaya data binafsi za jukwaa hilo kisiasa.
Mark Zuckerberg alijitetea kwa muda wa saa tano katika jopo la wasikilizaji kutoka bunge la seneti la Marekani linalohusika na masuala ya biashara na kamati ya mahakama.
Wakati wa hoja dhidi yakeBw Zuckerberg pia alisema:
  • "Ni wazi sasa kwamba hatukufanya juhusi za kutosha kulinda nyenzo zetu dhidi yakutumiwa kwa madhara"
  • "Ukiangalia mambo yalivyokwenda yalikuwa ni makosa ya wazi" kuamini kuwa Cambridge Analytica ilifuta data, bila kufanya uchunguzi zaidi
  • Hahisi "kama " Facebook ina udhibiti
  • Kwamba wakati wote kutakuwa na kitengo kisicholipiwa cha Facebook, kunachoweza kulipiwa , kitengo ambacho hakina matangazo ya biashara cha mtandao wa kijamii
  • Kukabiliana na kauli za uchochezi wa chuki " una kiwango cha juu cha makosa kuliko vile ninavyotaka "
  • Binafsi alihofia juu ya uwezekano wa upendeleo wa kisiasa kwneye kampuni yake utokana na hojaji hiyo hisa za mtandao wa Facebook jana ziliongezeka mpaka kufikia asilimia nne , nao wanasheria nchini Uingereza na Marekani wameanzisha mashtaka dhidi ya Facebook, Cambridge Analytica, na makampuni mengine mawili yanayounganishwa na kesi hiyo.
  • Na baada ya utetezi wake Mark ameelezea hisia zake kutokana na mtandao wa Facebook hapa ulipofikia na yanayojiri hafurahishwi na chochote.
    Utetezi wa Mark Zuckerberg, umepokelewa vyema na masoko ya hisa na hivyo kuifaidia Facebook kwa ongezeko la hisa asilimia nne  na nusu.

No comments:

Post a Comment

Mikoani leo

Mikoani leo