Aleyekuwa Mkurugenzi wa shirika la upelelezi nchini Marekani (CIA)Mike Pompeo |
Mkurugenzi wa shirika la upelelezi nchini Marekani Mike Pompeo alisafiri hadi mjini Pyongyang kwa mkutano wa kisiri na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un , kulingana na vyombo vya habari vya Marekani.
Mkutano huo ulioandaliwa kuandaa mkutano mwengine kati ya rais Donald Trump na Kim Jong Un ulifanyika wikendi ya sikukuu ya Pasaka , kulingana na maafisa amabo hawakutajwa.
Bwana Trump alikuwa amekiri kufanyika kwa mazungumzo ya hadhi ya juu na Pyongayng.
Lakini mkutano huo wa siri ambao haukutarajiwa ndio uliokuwa mkutano wa hadhi ya juu kati ya Marekani na Korea Kaskazini tangu 2000.
Tumekuwa na mazungumzo ya moja kwa moja , katika ngazi za juu'', Bwana Trump alisema mjini Florida ambapo alikuwa anakutana na waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe.
Rais huyo aliongezea kuwa aliunga mkono mazungumzo kati ya Korea kusini na kaskazini kuzungumzia makubaliano ya amani ya kumaliza vita vya Korea vya 1950-1953
Korea Kusini imetoa ishara kwamba itaangazia suluhu rasmi ya kumaliza mgogoro huo. Rais wa Korea Kusini Moon Jae in na bwana Kim wanatarajiwa kukutana.
Habari kwamba mteule wa rais Donald Trump katika wizara ya maswala ya kigeni alisafiri kueleka Korea Kaskazini kwa mkutano huo na bwana Kim ziliripotiwa mara kwanza na gazeti la The Washington Post.
Ni machache yanayojulikana kuhusu mazungumzo hayo mbali na kwamba yalilenga kuwa jukwaa la kuandaa mkutano mwengine wa moja kwa moja kati ya rais Donald Trump na Kim Jong Un.
Kulingaa na gazeti hilo, mkutano huo ulifanyika mara tu baada bwana Pompeo kuteuliwa kuwa waziri wa maswala ya kigeni kulingana na maafisa wawili waliokuwa na habari kuhusu safari hiyo.
Baadaye chombo cha habari cha Reuters kilisema kuwa ripoti hiyo imethibitishwa na maafisa waandamizi. Ikulu ya Whitehouse haijatoa tamko lolote.
Marekani haina uhusiano wa kidiplomasia na Korea Kaskazini lakini wajumbe wa mataifa hayo mawili wametembeleana miaka ya mbeleni na kuna idhaa zinazotumika kuwasiliana na Pyonyang.
Safari ya Bwana Pompeo ilikuwa ziara ya ngazi ya juu na kiongozi huyo wa Korea Kaskazini tangu 2000 wakati waziri wa maswala ya kigeni nchini Marekani Madeleine Albright alipokutana na Kim Jong-il, babake kiongozi wa sasa wa Pyonyang.
Mwaka 2014 , kiongozi wa shirika la upepelezi 2014, James Clapper alizuru Korea Kaskazini kisiri ili kujadiliana kuhusu kuwachiliwa huru kwa raia wawili wa Marekani .
Bwana Clapper hakukutana na kiongozi huyo wa Korea Kaskazini wakati wa ziara hiyo.
No comments:
Post a Comment