Mwili wa Mmiliki wa mabasi ya Super Sami Samson Josiah
umekutwa katika mto Ndabaka eneo la Bunda /Lamadi
Kwa mjibu wa Mtandao wa Jamii Forums ukinukuu taarifa kutoka kwa blogu ya Mwafrika Halisi zinasema kwamba mwili wa Samson Josiah umeokotwa na wavuvi wa samaki jioni ya Jumatano Machi 14,2018.

Watu wa karibu na marehemu wanasema mwili uliookotwa ni wa Samson Josiah.
Miongoni mwa habari zilizoteka vyombo vya habari Tanzania tangu Machi 9, 2018 hadi ni kuhusu kupotea kwa mmiliki wa mabasi ya Super Sami, Samson Josiah kwa zaidi ya wiki mbili sasa.
Mapema ilielezwa kuwa gari yake ndogo aliyokuwa akiitumia
aina ya Toyota LandCruiser ilikutwa imechomwa moto katika Hifadhi ya Taifa ya
Serengeti iliyoko mkoani Mara siku ya Machi 9, lakini yeye mwenyewe alikuwa
hajapatikana.
Kwa mujibu wa familia ya Bwana Josiah, ambayo inaishi mkoani Mwanza, ilidai kuwa siku ya kupotea kwa Josiah ambayo ni February 27, majira ya usiku, Josiah alimpigia simu mkewe na kumwambia kuwa atarudi nyumbani na mgeni, na hayo yakawa mawasiliano yao ya mwisho.
Mabasi ya Super Sami yanafanya safari zake kuanzia mkoa wa Mwanza, kwenda mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma, Iringa pamoja na Kagera.
Chanzo: Muafrika Halisi blog

No comments:
Post a Comment