Akiongea na
televisheni ya SABC ya Afrika kusini Mugabe amesema kuwa Rais wa sasa Emerson
Mnangagwa asingeweza kuingia madarakani bila kutumika kwa jeshi.
Akiwa katika
nyumba yake ya kifahari mjiniHarare Mugabe amekemea mbinu zilizotumika
kumuondoa madarakani.
Amesema
alikua tayari kufanya mazungumzo na Rais wa sasa Emerson mnangagwa na
angehakikisha mabadiliko ya madaraka ya uhalali na si yale ya kulazimishwa.
Mugabe
amesema kuwa Yuko tayari kwa ajili ya Mazugumzo na Mnangagwa ili kulinda katiba
yao.
Hakuna
uhakika kama rais huyo wa zamani mwenye Umri wa miaka 94 Anataka kurudi
madarakani ama la, lakini ni wazi kuwa anadhani amesalitiwa na rais wa sasa
Emerson Mnangagwa.
Amesema kuwa
hakudhani kama angepoteza imani yake kwa Mnangagwa kwani yeye ndie alimsaidia
kuingia serikalini.
“Siamini
kama yeye Mnangagwa angeweza kuniondoa madaraki , nimemuingiza serikalini,
nimemsaidia alipokua jela anataka kunyongwa, sikuwaza kabisa kama siku moja
yeye ndio atakua mtu wa kunitoa madarakani''.
Aidha Mugabe
ameogeza kuwa madaraka ya sasa yameingia kwa njia zisizo halali
''Lazima
tufute aibu hii, ambayo tumejiletea wenyewe, hatuistahili, hatuistahili,
hatuistahili , tafadhali hatuistahili kabisa.Tunatakiwa kuwa nchi inayoheshimu
katiba, ndio tunaweza kuwa na mapungufu hapa na pale lakini bado lazima
tuheshimu sheria.''
Katika
mitandao mbalimbali ya kijamii, baadhi ya wazimbabwe wanashangazwa na mkongwe
huyo wa miaka 94, na wengine wanaamini kuwa amepoteza uhalisia kabisa baada ya
kuongoza kwa miaka 38 , wakati wake sasa umekwisha.
No comments:
Post a Comment