Rais wa Zamani wa Liberia, Bi Ellen Johnson Sirleaf |
Ellen
Johnson Sirleaf amekuwa mwanamke wa kwanza barani Afrika kushika nafasi ya
Urais mwaka 2006 na kumaliza muda wake mwezi uliopita baada ya kuhudumu kwa
mihula miwili.
Kamati
ya Utendaji ya tuzo ya Mo Ibrahim imesema Ellen Johnson Sirleaf ameonesha uongozi
wa kipekee katika kukabiliana na changamoto zisizowahi kutokea katika awamu
zake mbili za uongozi alipokuwa Rais wa Liberia.
Wakati
aliposhinda uchaguzi wa Rais nchini humo mwaka 2005, nchi hiyo ilikuwa
imegawanyika kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa miaka
kadhaa na tuzo hiyo ya amani ilikuwa ni kwa ajili ya kumpongeza kusaidia
kuiimarisha nchi hiyo.
Mo Ibrahim |
Wakosoaji wake
wamekuwa wakimkosoa kwa kuwa na upendeleo, kutokana na kuwachagua watoto wake
katika nafasi za ngazi za juu na pia wanadai kuwa hakuchukua hatua za kutosha
kupambana na rushwa.
Kamati
yab utendaji ya Mo Ibrahimu imearifu kwamba inafahamu mapungufu yake, lakini
imeamua kwamba anastahili kupata tuzo ya dola za kimarekani milioni 5.
Mjasiriamali
Mwingereza mwenye asili ya Sudan Mo Ibrahim alianzisha tuzo hiyo mwaka 2007 kwa
ajili ya kuwatunukia viongozi walionesha kazi nzuri wakati wa kipindi cha
uongozi wao ndani ya bara la Afrika, amballo madikteta na watawala wadhalimu
wamerudisha nyuma maendeleo ya bara hili.
Tuzo
hii ambayo inapaswa kutolewa kila mwaka , kwa mara sita mfululizo ilishindwa
kupata mtu, kutokana na viongozi kukosa sifa za kushinda tuzo hiyo.
Ellen
Johnson Sirleaf atapata dola za Kimarekani milioni tano zitakazogawanywa kwa
miaka kumi, na dola laki mbili kwa maisha yake yote.
No comments:
Post a Comment