Joseph Kabla, Rais wa Congo- DRC (Picha ya Mtandao) |
Ajali
hiyo ilitokea wakati msafara wake ulikuwa ukielekea makao ya rais wa zamani
Keneth Kaunda eneo la Lusaka East.
Gari
dogo liligonga gari lililokuwa kwenye msafara wa rais ambapo vRais Kabila na
waziri wa mashauri ya nchi za kigeni Joe Malanji walikuwa, kwenye barabara ya
Leopards eneo la Woodlands.
Wote
hawakujeruhiwa.
Ripoti za awali zilisema
kuwa rais Edgar Lungu alikuwa kwenye gari lililopata ajali lakini zilikanwa na
ikulu ya rais.
Hii
ndiyo ajali ya pili ya barabarani kumkumba Kabila ndani ya wiki moja.
Wiki
iliyoptangulia watu watano waliuaawa wakati lori dogo liligonga msafara wa rais
nchini DRC.
Ripoti
zilisema kuwa wanajeshi watatu na raia wawili waliuawa kwenye ajali hiyo na
watu wengine 11 wakajeruhiwa.
No comments:
Post a Comment