Bwana Ombeta
amesema kuwa aliarifiwa kwamba bwana Miguna aliingizwa katika ndege iliokuwa
ikielekea Amsterdam na baadaye kuelekea Canada.
Wakili
mwengine Dkt. John Khaminwa alisema kuwa mteja wake tayari ameondoka Kenya.
"Ni
kweli .Alilazimishwa kuingia katika ndege ya KLM dakika chache tu kabla ya saa
nne usiku na tumebaini kwamba anaelekea Canada. Ni ukiukaji mkubwa wa haki'',
alisema Dkt Khaminwa kwa simu.
Haijulikani
ni sheria gani iliotumiwa na serikali kumuondoa nchini Kenya kwa kuwa katiba
inampatia haki kama raia wa Kenya kwa kuwa ni mzaliwa wa taifa hi
Anasema
kwamba wakati Miguna alipokamatwa , serikali ya Canada ilikuwa imeiandikia
Kenya kionyesha wasiwasi kwamba raia wake alikuwa ananyanyaswa na walitaka
arudishwe nchini humo.
Bwana Miguna
siku ya Jumanne alielezea vile alivyokamatwa bila mawasiliano na familia yake
ama wakili wake kwa siku tano.
Alisema kuwa
maafisa wa polisi walimnyanyasa kwa kumfungia katika maeneo ambayo hayafai kwa
binaadamu.
Bwana Miguna
alikuwa akizungumza katika mahakama ya kajiado ambapo alipelekwa baada ya
kukamatwa kwake siku ya Ijumaa kwa tuhuma za kushiriki katika sherehe ya
kumuapisha kiongozi wa upinzani Raila Odinga ambaye aliapishwa kuwa rais wa
wawananchi tarehe 30 Januari.
Ripoti za
kufurushwa nchini Kenya zilijiri saa chache baada ya jaji wa mahakama kuu Luka
Kimaru kumzuia mkurugenzi wa Ujasusi na inspekta jenerali wa polisi dhidi ya
kumwekea mashtaka yoyote.
Jaji
huyo awali alikuwa ameamuru kwamba inspekta jenerali wa polisi na mkurugenzi wa
shirika la ujasusi walikuwa wamekiuka agizo la mahakama lililowataka
kumwachilia kiongozi huyo.
Huku Jaji
huyo wa Kajiado akiagiza awasilishwe mbele ya jaji Kimaru katika mahakama ya
Milimani, bwana Miguna hakuwasilishwa katika mahakama hiyo huku mawakili wake
wakilazimika kusubiri hadi usiku wakisubiri kuachiliwa kwake.
Miguna
alikamatwa Ijumaa iliopita huku jaji wa mahakama kuu James Wakiaga akimwachilia
kwa dhamana ya ksh. 50,000 lakini hakuachiliwa.
Mkurugenzi wa
shirika la ujasusi baadaye alisema kuwa bwana Miguna alikamatwa baada ya kukiri
kumpatia kiapo kiongozi wa Nasa Raila Odinga mbali na kuwa mwanachama wa kundi
lililopigwa marufuku la NRM.
No comments:
Post a Comment