Mbunge wa Akadara George Aladwa |
Mbunge wa Makadara jijini Nairobi
George Aladwa alikamatwa asubuhi ya Jumamosi nyumbani kwake na maafisa wa idara
ya upelelezi na kupelekwa hadi makao makuu ya idara hiyo kwa mahojiano zaidi.
Aladwa ambaye amewahi kuwa meya
wa jiji la Nairobi, alikuwa katika mstari wa mbele katika mipango ya sherehe
hizo ambayo haikuwa na idhini ya serikali.
Aladwa sasa ni mbunge wa pili
kukamatwa kuhusiana na hafla hiyo ambayo pia imeshutumiwa na jamii ya
kimataifa.
Mbunge mwingine wa Nairobi Tom
Kajwang alikamatwa na kufikishwa mahakamani na hatimaye kuachiliwa kwa dhamana.
Mwanaharakati
mwingine wa upinzani wakili Miguna miguna pia alikamatwa siku ya Ijumaa na
angali anazuliwa na polisi licha ya mahakama kuruhusu kuachiliwa kwake kwa
dhamana.
Bwana Aladwa alikamatwa siku ya Ijumaa usiku katika
nyumba yake iliopo Buruburu kulingana na kiranja wa walio wachache bungeni
Junet Mohamed.
Bwana Mohammed ambaye pia mbunge
wa Suna Mashariki alisema kuwa bwana Aladwa kwa sasa anazuiliwa katika makao
makuu ya ujasusi.
Polisi hawajatoa tamko lolote
kuhusiana na kukamatwa kwa Aladwa.
No comments:
Post a Comment