Jumuiya ya Maimamu
Zanzibar imesema viongozi watano wa Dini ya Kiislamu wanadaiwa kutoweka katika
mazingira ya kutatanisha. Hii ni kwa mjibu wa tarifa iliotolewa
na Naibu katibu Mtendaji wa wa Jumuiaya ya Maimau Zanzibar Bw. Khamid Yusuf .
Jeshi la Polisi Zanzibar
limekana kuwakamata Viongozi hao kwa kusema hawako mikononi mwa Jeshi la
Polisi."Msijeanza sema ooh hao Polisi wameanza".’Amefafanua msemaji wa
Polisi ambaye hakuweza kufahamika jina lake mara moja.
Polisi wamesisitiza wanachi kutoa msaada wa kuwatafuta wakishirikiana na
Polisi.
Viongozi hao
ni Miongoni mwa Watu waliokuwa wakikusanya Michango kwajili ya Familia ya Mashehe ambao wapo ndani Gerezani kwa kipindi
kirefu.Michango hiyo nikwaajili ya familia zao ziweze kujikimu kimaisha.
Watu hao wamepotea toka
Ijumaa iliyopita,hadi leo hawajuilikani walipo.
Familia
za waliopotea wametoa taarifa Polisi na Polisi wanasema wanafuatilia lakini
hadi leo haijajuilikana wapo wapi.
Jumuiya
ya Maimamu ilalaani kitendo cha kupotea viongozi, Wanasiasa sababu wanaamini
Tanzania ina Vyombo vya dola ambavyo vipo imara,vina nguvu na uwezo
mkubwa.Kitendo cha watu kupotea ni cha kulaani.
Jumuiya ya Maimamu
haifurahishiwi na uvunjaji wa sheria wa nchi hii sababu hawajazoea hii hali ya
watu kupotea tu bila kujulikana, si taratibu za kisheria wala si taratibu za
kibinadamu.
Jumuiya ya Maimamu
inaunga mkono kitendo cha kukusanya fedha kwaajili ya kusaidia familia za
mashehe bila kujali wametenda kosa la Ugaidi au hawajatenda,kwa sababu sisi
tunaangalia familia za mashehe ikiwemo watoto wadogo wanataabika nyumbani bila
msaada.Hatuoni kama zile familia za mashehe zinazotaabika kama zina makosa.
Familia
zaidi ya 52 za Mashehe waliokamatwa ikiwemo watoto wadogo wanataabika.”Sisi
kama Waislam ni jukumu letu kuwasaidia.”
No comments:
Post a Comment