Jaji Charles Nyachae(Picha ya Mtandao/tuko.co.ke) |
Rais Kenyea, Uhuru Kenyatta amemteua Charles
Nyachae kuwa jaji wa Mahakama ya Haki
Afrika Mashariki(EACJ).
Mwenyekiti huyo wa zamani wa Kamati ya
Utekelezaji wa Katiba(CIC) anatarajiwa kula kiapo nchini Uganda.
Kulingana
gazeti la kampuni binafsi la Daily
Nation, limemnukuu msemaji wa ya Ikulu
ya nchi hiyo Bw. Manoah Esipisu kuwa
Nyachae ataapishwa wakati wa mkutano wa marais wa eneo la Afrika
Mashariki Kampala, Uganda.
Huenda likawa ikwa ndiyo ‘fadhila” kwani Nyachae alimfanyia kampeni Uhuru na
chama chake cha Jubilee wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Agosti 8 na uchaguzi wa
marudio wa Oktoba 26.
Chama cha Jubilee kiilimteua kama mbunge wa
Bunge la Afrika Mashariki(EALA) lakini jaji huo alikataa ofa hiyo ya kuchaguliwa.
Nyachae alipoteza wadhifa wa useneta kwenye Kaunti ya Kisii baada ya kushindwa na Prof
Sam Ongeri(ODM) wakati wa uchaguzi wa Agosti.
No comments:
Post a Comment