Hussein Bashe, Mbunge wa Nzega,
|
Bashe ameyasema leo Februai 24 wakati akishiriki mjadala kwenye kipindi cha Meza ya Duara kinachorushwa na Idhaa Ya Kiswahili ya Radio Dw.
"Kama taifa kunahitajika mjadala ili kutaka demokrasi tuipendayo ili tusivunje umoja wetu wa siku nyingi" amesema Bashe
Mbunge huyo machachari kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) amesema kuwa taasisi zilikabidhiwa dhamana ya kuongoza na kusimamia demokarisia zinapaswa kutokwenda kinyume na utaratibu ili kuleta usawa.
Aidha Bashe amesema kuwa katika kujenda nchi ni lazima tukosoane na kukubali kukosolewa na wanaokosoa wakosee kwa hoja na si ushabaiki na utashi wa kisiasa au kundu fulani wanaloliongoza
" Tunapojenga nchi tukubali kukosolewa na wanaokosoa wafanye hivyo kwa hoja bila kuwa na maslahi ya kikundi wanachokiongoza au kwa masilahi ya kisiasa.
Mbunge huyo kijana amesema kuwa Tanzania ni ya Watanzania na CCM haina hati miliki ila imepewa dhamana ya kutawala.
Mjadala huo wa meza ya duara ulikuwa na maada kuu matukio yanayoendelea kutoka kutaka na chaguzi hapa Tanzania na maana hasa ya Demokrasia tangu mwaka 1992 na changamoto zake
No comments:
Post a Comment