Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma(getty Image) |
Kwa
mujibu shirika la Utangazaji la Afrika Kusini -SABC- na vyanzo vingine vya
habari, hatua hii inakuja baada ya mlolongo wa mazungumzo yaliyofanywa na chama
tawala cha nchini humo ANC.
Duru
zinasema ANC kilifanya mazungumzo marefu ya takribani saa 13baadaye kuwatuma watu wawili nyumbani
kwa Rais Zuma jijini Pretoria kwenda kumfikishia ujumbe wa chama ana kwa ana ya
kwamba Zuma ajiuzulu mwenyewe au chama kimng'oe madarakani.
Lakini
haijulikani bado kwamba Rais Zuma alipokeaje ujumbe huo.
Baadhi ya wanachama wa ANC(Getty Image) |
Hatua hii ya ANC
inaonekana ndio njia rahisi zaidi ya chama hicho kumng'oa rais Zuma madarakani
badala ya kusubiri utaratibu wa bunge ambao ungeweza kuwa mrefu na wenye
madhara zaidi kwa chama cha ANC.
Rais
Jacob Zuma ambaye anakabiliwa na mashtaka kadhaa ya rushwa, alishindwa uongozi
wa chama tawala Desemba mwaka jana.
Kiongozi
mpya wa ANC, Cyril Ramaphosa anaongoza shinikizo za kumuondoa Zuma katika
nafasi yake hiyo ya Urais, na hatimaye kushika pia nafasi hiyo.
Ramaphosa
ameahidi pia kupambana na rushwa iliyokithiri na kukijenga upya chama cha ANC,
wakati nchi hiyo ikielekea katika uchaguzi mwakani.
No comments:
Post a Comment