Ni tambo za hapa na pale wakati timu 2 maafuru hapa nchini zikimenyana leo Januari 27, 2018 kwenye mwendelezo wa ligu kuu Tanzania Bara (VPL)
Timu ya Azam FC, chini ya kocha Mromania,
Aristica Ciaoba, kinachowakabili mabingwa watetezi Yanga, katika Dimba lao la Azam . Azam Complex enelo la Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaaam kwanzia majira ya saana 10: 00 jioni
Hiyo ni mara ya kwanza kwa timu hizo kukutana msimu huu, na kila upande
umejitapa kushinda mchezo huo ili kujiweka katika nafasi nzuri kwenye msimamo
wa ligi hiyo inayoshirikisha timu 16.
Wenyeji Azam wapo katika nafasi ya pili kwenye msimamo wakiwa na
pointi 30, na wataingia kwenye mchezo huo kwa nguvu kubwa baada ya ushindi wa
mabao 2-0, walioupata Jumapili iliyopita dhidi ya Tanzania Prisons kwenye
Uwanja wa Sokoine, Mbeya.
Mbali na ushindi huo, lakini Cioaba, atakuwa anafurahia kurejea
wa washambuliaji wake wawili, Mbaraka Yusufu na Wazir Junior waliokosa mechi za
Kanda ya Ziwa kutokana na majeruhi, huku pia safu yake ya ulinzi ikizidi
kuimarika baada ya beki Mghana Daniel Amoah kurejea kikosini.
“Naiheshimu Yanga kwa sababu ni timu kubwa yenye historia nzuri
na ndiyo mabingwa watetezi, lakini mchezo wa kesho tumejipanga kuhakikisha
tunachukua pointi zote tatu,” alisema na kuongeza:
“Nafurahi maandalizi yetu
yanakwenda vizuri na wachezaji wote wapo fiti kwa ajili ya mchezo huo ambao
tumepania kuonesha ubora na dhamira yetu ya kutaka ubingwa,” alisema Cioaba.
Kwa mupande wao Yanga kupitia kwa kocha wao mkuu George
Lwandamina, amesema mchezo utakuwa mgumu, lakini lengo lao ni kuhakikisha
wanashinda ili kuzidi kuzikimbiza Simba na Azam zilizopo juu yao.
Lwandamina alisema wachezaji wake wote wapo vizuri na wana
usubiri kwa hamu mchezo huo baada ya kufanya mazoezi makali wiki hii kwenye
Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.
Lwandamina atamkosa kiungo mshambuliaji Pius Buswita, lakini
ameonekana kuwa na furaha baada ya kurejea kwa mshambuliaji wake anayeongoza
kwa mabao Obrey Chirwa, aliyemaliza adhabu yake ya kufungiwa mechi tatu na beki
Kelvin Yondani ambaye alikosa mechi iliyopita baada ya kuwa na kadi tatu za
njano.
“Tumejipanga kuhakikisha hatupotezi pointi nyingine najua presha
ni kubwa, lakini kitu cha msingi kwetu ni pointi tatu ili kurudisha matumaini
ya ubingwa kwa mashabiki wetu,” alisema Lwandamina.
Kocha huyo huenda leo akaendelea kutokuwepo katika benchi la
Yanga na akakaa jukwaani endapo Yanga watakuwa hawajafanikiwa kupata kibali
chake cha kikazi.
Wenyeji Azam wanahitaji ushindi ili kuendelea kuifukuza Simba
iliyopo kileleni wakitofautiana kwa pointi mbili na kama ikishinda itaongoza
ligi, huku ikisikilizia mchezo wa Jumapili kati ya Simba na Majimaji.
No comments:
Post a Comment