Rais wa Marekani Donald Trump amesema kuwa Bara la siyo chafu kama alivyotafasiriwa hapo awali.
Bw Trump amekanusha kwamba
alitumia neno hilo kuyaelezea mataifa ya Afrika.
Viongozi
hao wawili wamekutana mjini Davos, Uswizi pambezoni mwa mkutano wa viongozi na
watu mashuhuri kuhusu uchumi na biashara duniani.
Mkutano
huo wa Kagame na Trump umetokea wiki chache baada ya kiongozi huyo wa Marekani
kuyaeleza mataifa ya Afrika kama "machafu" au mataifa ya
"mabwege".
Hata
hivyo alikiri kwamba alitumia maneno makali akiyaeleza mataifa ya Afrika, Haiti
na El Salvador alipokuwa anazungumzia wahamiaji wanaoingia Marekani.
Lakini
katika mkutano wake na Kagame pambizoni mwa Mkutano wa Uchumi wa Dunia mjini
Davos, Trump hajaonyesha dalili zozote za majuto kuhusu tamko lake la awali
kuhusu Afrika.
Ameongeza:
"Ningependa kukupongeza, Bw Rais, unapochukua majukumu ya kuwa kiongozi
mpya wa Umoja wa Afrika, ni heshima kubwa … najua unaenda kuhudhuria mkutano wa
kwanza karibuni. Tafadhali, fikisha salamu zangu."
Rais
Kagame alisema wameshauriana kuhusu ushirikiano wa nchi hizo mbili, ikiwa ni
pamoja na usaidizi wa Marekani kwa Rwanda katika "operesheni zake kote
duniani", pamoja na masuala ya kiuchumi, biashara, uwekezaji na idadi ya
watalii wa Marekani wanaozuru Rwanda, ambayo inaongezeka.
Mkutano
wa viongozi wa nchi wanachama wa AU utafanyika Jumapili na Jumatatu
No comments:
Post a Comment