Jacob Zuma, Rais wa Afrika Kusini |
Hapo jana usiku viongozi wa chama cha ANC walitangaza kwamba
wataitisha mkutano wa kiwango cha juu wa kamati ya kitaifa NEC kuondosha mzozo
wa kisiasa kwa lazima.
Mkutano huo unaotarajiwa siku ya Jumatano unatafanyika siku moja
kabla ya hotuba ya bunge ya kila mwaka anayotarajiwa kuitoa Zuma bungeni.
Matarajio ni kwamba NEC itapiga kura kumuondoa madarakani.
Lakini Zuma anaweza kwenda kinyume na matakwa ya chama. Hilo
basi litaweza kuzusha uwezekano mkubwa na ambao haujawahi kufanyika wa wabunge
wa ANC kumpigia kura ya kutokuwa na imani naye.
Kauli ya chama cha ANC iliyotolewa kuhusiana na mkutano huo imesema
kuwa, wanakutana kujadili ubadilishanaji madaraka kutoka Rais Zuma kama
mwenyekiti wa zamani na sasa Cyril Ramaphosa ambaye ni kiongozi mpya wa chama
hicho.
Siku ya jumatatu viongozi wandamizi wa chama hicho walilazimika
kuwa na mkutano wa dharula mjini Johannesburg kujadili hatima ya rais Zuma.
Hata hivyo rais Zuma ameshikilia msimamo wake kutokubaliana na
shinikizo la kumtaka aachie madaraka.
Mwezi Disemba mwaka jana Ramaphosa alimrithi rais Zuma katika
nafasi ya juu ya kukiongoza chama hicho kikongwe barani Afrika.
Rais Zuma amekuwaakiandamwa na kashfa za rushwa, ambapo katika
miaka ya hivi karibuni alihusishwa na familia yenye asili ya India ijulikanayo
kama Gupta - ambapo inadaiwa alitumia madaraka yake vibaya ili kujinufaisha
yeye na washirika wake hao.
No comments:
Post a Comment